Peter Msechu amesema kauli yake ya hivi karibuni kuwa kama wimbo wake aliomshirikisha Amini ‘Nyota’ usingefanya vizuri angeacha muziki, ilitaka kumponza kwakuwa alisema kwa utani tu na watu wakaichukulia kwa uzito mkubwa.
Msechu amesema kuwa baada ya kutoa kauli hiyo alipokea simu nyingi kutoka kwa watu waliotaka kujua kama kweli amedhamiria. “Unajua niliongea vile kwakuwa nilikuwa naiamini sana hii nyimbo. Lakini unajua nilihisi ile kauli kama ilianza kunikosti japo niliongea kawaida maana nilipata simu nyingi sana kuhusu hiyo kauli hadi nikahisi yaani hii nyimbo isipofanya vizuri itakula kwangu,” amesema Msechu. “Lakini nashukuru Mungu katika nyimbo zangu zote ambazo nimewahi kutoa, ‘Nyota’ ni nyimbo ambayo inafanya vizuri sana ndani na nje ya nchi. Kama sasa hivi kuna redio ipo Rwanda ipo katika top ten na imeshika namba tano. Na pia Kenya inapendwa sana. Hii yote inatokaNA na kufuata ushauri. Nakumbuka Bongo5 kuna waraka mliwahi kuandika niliufanyia kazi ndo mana nikaamua kumtafuta Amini tukakaa chini tukasaidiana kuaadika. Ila sehemu kubwa sana kafanya Amini. Nilimuachia yeye kwakuwa namkubali sana na pia nikaona ili nipate ladha tofauti basi nimuachie yeye. Ndo maana unaona nimebadilika sana. Kwahiyo mashabiki wangu wakae tayari kwa video inatoka hivi karibuni. Na pia Mungu akijalia uzima mwezi wa 11 naachia nyimbo nyingine.”
Kwa upande mwingine Msechu ameeleza kuhusu ukaribu alionao na msanii mwenzake wa Kigoma Allstars, Baba Levo.
“Unajua kwanza mie na Baba Levo wote tumetoka sehemu moja Kigoma. Wakati Baba Levo kaanza muziki mie nilikuwa bado nipo naimba kanisani ila nilikuwa namsikiliza sana na pia nilikuwa shabiki wake sana enzi izo Baba Levo alikuwa anajiita OBD na alikuwa anafanya vizuri sana Kigoma. Na mie nilivyo ingia kwenye muziki huu nikajikuta tumekutana na tukawa marafiki wakubwa sana kiasi cha kwamba hadi tumekuwa kama ndugu. Na tukiwa pamoja lazima watu wacheke sana. Kwahiyo mashabiki wetu wategemee kupata kazi ya pamoja ya mie na Baba Levo. Kuna vitu vinakuja vizuri sana japo sasa hivi bado mapema sana kuviongelea. Kwahiyo wakae tu tayari wataona. Na pia tutakuwa pamoja katika steji ya Fiesta Iringa mie na Baba Levo, wategemee kupata kitu tofauti na walivyozoea.”

0 comments :
Post a Comment