Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS, JAJI ASEMA HANA ATIA KATIKA MASHTAKA YA KUUA BILA KUKUSUDIA

KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS, JAJI ASEMA HANA ATIA KATIKA MASHTAKA YA KUUA BILA KUKUSUDIA



Hatimaye Jaji Thokozile Masipa ametoa maamuzi juu ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius na kutupilia mbali madai kuwa aliua kwa kukusudia.

Baada ya muda mrefu na mgumu wa muenendo wa kesi hiyo, jaji huyo ameamuru kuwa Pistorious hana hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili.

Jaji Masipa ameeleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Oscar alimuua mpenzi wake kwa kukusudia baada ya kuwepo ugomvi kati yao.

Hata hivyo, jaji Masipa ameeleza kuwa ameridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka kuwa Oscar Pistorius alikuwa na uwezo wa kutambua mabaya na mema wakati wa tukio hilo.

Huenda mwanariadha huyo akafunguliwa shitaka la kuua bila kukusudia baada ya kuyavuka mashitaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo.

Oscar Pistorius alimuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka 2013. Lakini katika utetezi wake aliiambia mahakama kuwa alimpiga risasi kimakosa akidhani ni mtu aliyevamia katika nyumba yao usiku ule.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX