Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » MAINDA AFUNGUKA JUU YA UGUMU WA KUACHA MKOROGO...

MAINDA AFUNGUKA JUU YA UGUMU WA KUACHA MKOROGO...

STAA wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vilivyokuwa vimeuteka ujana wake ni pamoja na matumizi ya mkorogo ambapo ilikuwa vigumu kuacha baada ya kuokoka.

Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema kutokana na starehe za ujana pamoja na kutaka kuonekana mrembo, alitumia vipodozi hatari bila kujua kwamba vina madhara makubwa mwilini mwake.
Kusema kweli niliamini mkorogo ni kitu ambacho kingeniongezea mvuto kwa kiasi kikubwa, bila kujua kuwa nilikuwa najisababishia madhara mwilini.
Pia nilikuwa nafanya kitu kisichompendeza Mungu, katika kujitakasa na maovu yangu kwa Bwana ndiyo maana nikaamua kuacha kabisa kujichubua japo haikuwa rahisi,” alisema Mainda.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX