Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Meneja wa Diamond Afunguka Kilicho Sababisha Diamond Asifanye show London Juzi Usiku

Meneja wa Diamond Afunguka Kilicho Sababisha Diamond Asifanye show London Juzi Usiku

Kutokana na tukio hilo, Meneja wa mwanamuziki huyo, Hamis Taletale maarufu Babu Tale ambaye hakuambatana naye, aliliambia gazeti hili kuwa Diamond alipokea mwaliko kutoka kwa promota huyo, lakini hakulipwa fedha hata kidogo, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya uamuzi wowote.

“Diamond alipofika Uingereza yule promota alimdaka juu kwa juu kwa kuwa kule alikwenda kwa ajili ya shoo ya Ujerumani itakayofanyika usiku wa leo (jana) akimtaka afanye shoo jijini London, Uingereza, alikubali na baada ya hapo alisema kuwa angemlipa siku ya shoo, lakini kwa wakati wote hakufanikiwa kuonana naye tena, alikuwa akiwasiliana naye kwa simu tu,” anaeleza Taletale.
Alisema Diamond alimsubiri promota huyo kwa muda mrefu, licha ya kufanya matangazo aliamini kuwa kabla muda wa shoo haujafika angemlipa fedha ili aende ukumbini.
“Diamond alishangaa kuona ilipofika saa nne usiku wa kuamkia jana promota yule hapatikani, kwa kuwa hakulipwa hata dola moja (Sh1,600) aliamua kutulia hotelini kwani promota ndiye anatakiwa amfuate msanii, na yeye hakufanya hivyo wala hakumlipa hata kidogo. Msanii wangu hana makosa ndiyo sheria ya kazi ilivyo,” alisema Taletale.
Hata hivyo, Taletale alisema wamiliki wa ukumbi ndio walioamua kuita polisi baada ya kuona viashiria vya vurugu, na hapo ndipo ilipogundulika kuwa promota huyo hakulipia ukumbi pia.
“Licha ya kwamba hakumlipa msanii wangu, pia ukumbi hakuulipia. Alichokifanya mmiliki ni kurudisha fedha kwa watu waliohudhuria mbele ya polisi na promota yule akakamatwa.”
Akizungumzia usalama wa Diamond, Taletale alisema, “Msanii wangu yupo katika mikono salama na hivi tunavyoongea ameshapanda ndege kuelekea Ujerumani kwa ajili ya shoo jioni ya leo. Hana kosa lolote, hakuna mkataba baina yake na promota unaoonyesha kwamba alilipwa,hivyo hakuwa na kizuizi na polisi hawajashughulika naye,” alisema Taletale.
Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini anamwacha msanii wake asafiri peke yake na kufanya makubaliano na mapromota kazi ambayo alitakiwa aifanye yeye (Taletale) alisema:
“Ilikuwa nisafiri naye, lakini kwa bahati mbaya kulikuwa na matatizo ya kifamilia ambayo ilinilazimu nibaki nchini. Yeye alikwenda kwa ajili ya shoo mbili zilizofanyika Jumamosi Afronation na hii ya leo itakayofanyika Sturtgart. Huyu promota alimdaka tu,” alisema Babu Tale.
Baada ya kutokea kwa vurugu hizo, mwanamuziki Diamond alisema promota huyo amemtapeli kwa kuwa hayakuwa makubaliano yao awali.
“Tafadhali ndugu zangu wa Uingereza haikuwa dhamira yangu, kuweni makini sana na promota huyu Victor Dj Rule, mnaposikia kaandaa shoo, pati au hafla yoyote ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwa sababu ni tapeli, si unajua aisifiaye mvua imemnyeshea, basi miye nimeloa kabisa,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Akizungumzia sakata hilo, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba alisema tatizo alilopata Diamond limepokewa kwa masikitiko makubwa na wanamuziki wote nchini.
“Tunasikitika kwani hii ni mara ya pili inatokea tena kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini baada ya kufanya mawasiliano, tumegundua tatizo lilikuwa la promota, mwanamuziki wetu hana hatia na ameshaondoka Uingereza leo (jana) asubuhi na sasa yupo Ujerumani kwa ajili ya shoo nyingine ya usiku wa leo,” alisema Ado.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX