Wakili wa watu hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikimaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo. Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjini Tehran.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja. Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.
Kanda hiyo kwa jina, “Happy we are from Tehran” ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye YouTube. Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Pharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao. “Inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Source:BBC
0 comments :
Post a Comment