Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
“Sasa akiwa pale baa, alizidi kunogewa na masaa yalizidi kupotea
ndipo Zeno alirudi nyumbani na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo
huku akisikia harufu kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,” kilidai chanzo hicho.
AMUIBUKIA BAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia ‘kunyonya’ kilevi kikali.
ZACHAPWA
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya kuzidiwa na kilaji.
LAHAMIA NJE YA BAA
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
WARUDI NYUMBANI
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
ETI WAMEYAMALIZA!
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.
0 comments :
Post a Comment