Filamu ya Kitanzania iitwayo ‘Dogo Masai’, imetajwa kuwania tuzo
za Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) za nchini Marekani.
Filamu hiyo imetayarishwa na kuongozwa Timoth Conrad Kachumia, wa
Timamu African Media.
Dogo Masai imeingia kwenye kipengele cha Best Feature Film ambapo
inashindana na filamu kutoka katika nchi mbali mbali zikiwemo Afrika
Kusini, Malawi, Misri, Nigeria, pamoja na Uganda. “Kutoka nchini
Tanzania Dogo Masai ni filamu pekee ambayo imeingia kwenye mashindano
hayo, lakini kwa East Africa ni filamu mbili ambayo moja ni kutoka
Uganda na hapa kwetu,” amesema Timoth.
Kuona list nzima ya filamu zilizochaguliwa kushindana na DOGO MASAI fungua mtandao hapa.
Licha ya kufanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo za Marekani, lakini pia
Filamu hiy imechaguiwa kuingia kwenye tamasha la Rome Independent Film
Festival (RIFF) la nchini Italia.
Ingia hapa kuona.
Si mara ya kwanza kwa Timoth kuandaa filamu ikaingia kwenye tuzo
kubwa barani Ulaya. Mwaka mwaka jana Timoth Conrad alihusika katika
kuandaa filamu iliyoitwa Mdundiko iliyoongozwa na Jackson Kabirigi. Nayo
ilileta heshima nchini baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo hizo za SVAFF
ambazo zinaandaliwa nchini Marekani. Licha ya kunyakua tuzo hizo lakini
pia ni filamu ambayo ilipata nafasi ya kuchaguliwa kushindana kwenye
tuzo nyingi barani Africa na kwingineko.
DOGO MASAI ni filamu ya kitanzania inayomuelezea kijana Dogo masai
ambaye anaamua kuuvaa uhusika wa kuwa muonekano wa kimasai baada ya
kufanyiwa vitendo vya kinyama na mjomba wake. Hivyo anaingia katika
safari ndefu ya kutafuta suluhisho la yote aliyofanyiwa. Ni filamu ya
kusisimua na kuhuzunisha pia kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao
Dogo Masai.
Wahusika kwenye filamu hiyo ni pamoja na Omary Clayton, Hissani Muya, Mainda Suka, Julieth Samson na Mukasa Tabani.
0 comments :
Post a Comment