Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Hiki ndicho Kilichomfanya Jacqueline Wolper Aifute Hii Picha ya Lucy Komba Instagram

Hiki ndicho Kilichomfanya Jacqueline Wolper Aifute Hii Picha ya Lucy Komba Instagram



 
September 17 2014 mwigizaji Jackline Wolper aliweka kwenye page yake ya Instagram picha ya mwigizaji mwenzake Lucy Komba alieolewa hivi karibuni na raia kutoka nje ya Tanzania na kuandika masikitiko yake ya kushindwa kuhudhuria harusi hii.
Wolper aliandika ‘Tukio lililoniuma ni kutohudhuria katika furaha ya milele ya my dada kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu‘ ambapo baada ya post hiyo baadhi ya followers wa Wolper walianza kutukana kwenye comments na kukosoa mavazi ya Maharusi kama unavyoona hapa chini.


Baada ya matusi kuongezeka ilibidi Wolper aifute hiyo post muda mfupi baadae na kisha akapost picha yake na kuiambatanisha na haya maneno >>> ‘Jamani hivi wapenzi wa Insta tabia ya mimi kuweka picha ya mtu alafu mnakosoa mnatukana sio poa, kwanini msitukane yangu tuu, naweka picha za maharusi wa watu mnaweza kuwa Wanamitindo wa kukosoa watu hawajui kuvaa kwanini? sio poa sijapenda…… haya nibomoeni hapo hiyo picha ni yangu, ruksa‘

 
Hata hivyo baadae ya hii post Wolper alipost nyingine ya Maharusi hao lakini isiyoonyesha sana mavazi yao kwa kiasi kikubwa ambayo ndio hii hapa chini na kuandika maneno mafupi tu…. ‘One love my sisy’

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX