Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea
maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo
inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi
umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa
mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji
wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba
ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya
kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa
katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi
kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za
kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa
kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na
makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu
kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema
wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea
mtazamo wa mtandao wa Facebook.
0 comments :
Post a Comment