Wanamgambo wa islamic state wametoa video nyingine inayomuonyesha mwandishi wa uingereza John Cantlie aliyekuwa ametekwa nyara.
Cantlie akiongea katika video hiyo ya dakika sita amesema alikuwa
ametelekezwa na serikali yake na kwamba nchi za Magharibi zilikuwa
zimepuuza uwezo wa wanamgambo wa IS.
Cantlie alitekwa huko syria mwaka 2012 ,na video yake inafanana na ile
iliyotolewa wiki chache zilizopita ambapo alisema alikuwa ni mmoja wa
wafungwa katika kundi.
IS tayari imeua mateka watatu wa nchi za magharibi na wamenuia kuua
waingereza wanaofanya kazi ya kutoa misaada wanaowashikilia mateka.
0 comments :
Post a Comment