Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » YOUNG KILLER AFUNGUKA GHARAMA ALIYOTUMIA KUFANYA VIDEO YA "UMEBADILIKA"..SHUKA NAYO HAPA KUJUA

YOUNG KILLER AFUNGUKA GHARAMA ALIYOTUMIA KUFANYA VIDEO YA "UMEBADILIKA"..SHUKA NAYO HAPA KUJUA

Young Killer amesema ametumia gharama kubwa kufanikisha kushoot video ya wimbo wake ‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro.



Killer amesema kuwa zaidi ya shilingi milioni nane zimetumika hadi kuikamilisha. “Ni video ambayo nimeingia gharama kubwa, tofauti na video zote nilizowahi kuzifanya,” amesema rapper huyo. “Yaani ukianza kulinganisha video zangu ambazo zimepita nadhani kwa hii video inafikia katika maandalizi tu yaani sio hela ya kumlipa director ni kama milioni nne.”

Young Killer amesema ili kwenda kushoot video hiyo kisiwani Mbudya ilimlazimu kukodi boti kwa siku mbili.

“Hiyo ni kwenye mtumbwi tu, bado kuna ngalawa mle, tulikodisha ngalawa kushoot sehemu za Banana. Kuna watu waliocheza mle wamehitajika kulipwa, kuna majengo ya zamani tuliyakodisha, nauli za hapa na pale, watu wanahitaji wale,” ameongeza.

Rapper huyo amesema video hiyo ni kali kuliko hata anavyoisema mdomoni. “Naamini watakayoiona itakuwa kali zaidi ya hii ninayoisema.”

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX