KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai
alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa
Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Paka
mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti
uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo,
Morogoro.
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo
lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa
msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.
Baadhi ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema
alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo
uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji
Mpya.
“Tulifika hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa
bado kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa
kupiga kelele mfululizo.
“Tuliposogelea tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi. Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.
“Tuliposogelea tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi. Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.
“Unajua eneo hili lina miti mingi lakini wahusika wamekuja kumpigilia
misumari paka huyu hapa. Mimi nasema wasakwe hawa watu tuwajue,” alisema
muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Said.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya msikiti huo, Haji Said Dihole alipohojiwa na mwanahabari wetu alisema:
”Kama kuna mtu alitaka kutujaribu angemuweka paka huyo kwenye eneo letu la msikiti angeipata habari yake, pia nasikia tukio kama hili liko kwa majirani wetu pale Kanisa la T.A.G Mwembesongo, nenda kashuhudie.”

Baaada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi
kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God ‘T.A.G’ linalofahamika kwa
jina la Bethel Revival Temple lililopo Mwembesongo.
0 comments :
Post a Comment