Shirika la Viwango (TBS) limewataka wananchi kutonunua nguo za ndani za mtumba ili kuua soko la bidhaa hizo zenye athari kiafya.
Kaimu mkurugenzi anayehusika na udhibiti ubora wa TBS, Mary Meela alisema nguo hizo ni hatari kwani zinaweza kueneza magonjwa mbalimbali hasa ya ngozi.
Alisema lengo la ombi hilo ni kukomesha uuzaji wa nguo hizo ambazo zinaweza kusababisha maambukizi kutoka kwa aliyekuwa anavaa nguo hiyo kwenda kwa mtu wa pili.

“Nguo za ndani zina bei ndogo hata mtu wa chini anaweza kumudu. Sioni sababu ya mtu kwenda kununua za mtumba,” alisema.
0 comments :
Post a Comment