MAHABA niue! Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo
Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka
kwenye mitandao ya kijamii huku akimmwagia sifa kemkem.
Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya,
Hamisa alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana
malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka
hadharani soon!
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.
Mtoto mzuuuuri... kunako fani ya mitindo Bongo, Hamisa Mabeto akipozi.
“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote
kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,”
alisema Hamisa.
0 comments :
Post a Comment