Amani! Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa kuwa yuko mbioni
kuhukumiwa kwenda jela huko Dubai, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel
Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa
muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Staa
wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini
Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati anaondoka nchini hivi karibuni, Aunt alionekana kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, akiwa na mwanaume
ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari
hiyo kuripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda, Septemba
15, mwaka huu, ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa
na kitendo hicho.
Wakipata msosi.
“Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko
anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa
kweli,” alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina
lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.

Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
“Kassim aliambiwa atafute kampani ya kuja nayo huku ndipo akaona Aunt
anafaa kwa kuwa mwenyewe amedai ni mtu wake wa karibu,” kilisema chanzo
hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.

Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson.
Baada ya mwanahabari wetu kunasa mchapo huo, alimtafuta Aunt kupitia
WhatsApp hakupatikana, bahati nzuri Kassim alipatikana na
kusema:“Tumekuja kwa mwaliko wa ubalozi wetu, Aunt ni mshkaji wangu kwa
hiyo usishangae sana nikila naye bata,” alijibu Kassim.
0 comments :
Post a Comment