Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Ben Pol adai uhusiano wa miezi 9 na Latifa ni mrefu zaidi aliowahi kuwa nao tangu awe staa


Uhusiano na mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2013, Latifa Mohamed wenye miezi tisa sasa, ndio uhusiano mrefu zaidi aliowahi kuwa nao Ben Pol tangu awe staa.

Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa mahusiano yake yaliyopita yalishindwa kudumu kwakuwa wasichana wengi walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwake kwakuwa yeye ni msanii. “Sasa hivi tuna miezi tisa, nadhani ndio the longest relationship,” amesema Ben kuhusu uhusiano na Latifa.

“Unajua nimekutana na watu wa aina tofauti. Nimekutana na watu ambao labda wanakuwa na expectations kubwa zaidi kuhusu mtu fulani, kwahiyo akiingia kwenye maisha yako labda kuna vitu ambavyo yeye tayari alishapicture, ‘labda Ben Pol tutakuwa tunakula bata every weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku kule everyday. Kwahiyo mtu anaweza akaja kwenye maisha yako akakuta sio mtu wa hivyo, ni staa ndio lakini you don’t go to clubs mara kwa mara, you don’t do this, you don’t do that kama mastaa wengine. Kwahiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye maisha yako. Ndio hicho ambacho nimeexperience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita.”

“Kwahiyo ukipata mtu ambaye akakuelewa hivyo, inatia moyo kidogo.”

Ben Pol amesema hata hivyo uhusiano wake na Latifa haujawa rasmi kabisa kwakuwa bado hajaenda kujitambulisha kwao.

“Lakini at least naweza kusema nina hatua moja katika tano au katika tatu.”
-Bongo5

Uzuri Wamponza Dada Huyu, Wenzake Wamuonea Wivu na Kumrarua Sura

WASICHANA ndugu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 na 18 wamemshambulia kwa visu binti mwenye miaka 15, kwa lengo la kumkomesha kwa sababu anasifiwa kuwa mzuri. 

Katika tukio hilo la aina yake, ndugu hao walimvizia msichana huyo, Julia Alvarez(15), njiani wakati anakwenda nyumbani mjini Juan Domingo Peron kwenye jimbo la Formosa Kaskazini mwa Argentina.

Kwa mujibu wa kauli za wasichana hao, walifanya unyama huo kwa kuwa hawakupenda kusikia sifa alizokuwa anapewa binti huyo kuwa ni mrembo sana.

Mwathirika huyo, Alvarez alisema wakati anashambuliwa, wasichana hao walisema, walitaka kumharibu awe anatisha kama mcheza sinema za kutisha, Chucky.

Msichana huyo alisema alivamiwa wakati anakwenda nyumbani kujiandaa kwenda kuwatembelea rafiki zake, wasichana wawili walimvamia, wakaanza kumpiga na kumwangusha chini. Alvarez amesema, baada ya yeye kuanguka, wasichana hao walitoa visu na wakasema,

“Kila mtu anasema una mvuto, tukikumaliza mvuto wote utaisha, watu watakuita Chucky”. Mtoto huyo alikatwa kwa visu kwenye sehemu mbalimbali mwilini hasa usoni na mgongoni. Baada ya kumuumiza binti huyo, wasichana hao walikimbia na kumwacha amelala kwenye dimbwi la damu, mpita njia alimwona, akamkimbiza hospitali.
Inadaiwa kuwa, awali polisi hawakuchunguza tukio hilo lakini dada wa majeruhi aliweka picha za mdogo wake kwenye mtandao wa facebook, ndipo watu wakashinikiza haki itendeke. Wasichana waliomshambulia Alvarez wakamatwe.

“Walimwonea wivu mdogo wangu kwa muda mrefu, na kila mara walimkashifu na kumtukana lakini hatukutarajia kufika mbali kiasi hiki. Nimejaribu kuwa mvumilivu kwa ajili ya mdogo wangu mrembo lakini kila mara nikimwona nataka kutokwa machozi, wameharibu maisha yake,” amesema mwanamke kwenye ukurasa wa facebook akijitambulisha kuwa ni dada wa binti aliyejeruhiwa.

“Alisema anataka kujiua kwa sababu sasa akijitazama kwenye kioo anajiona mbaya, imeharibu familia yetu,” alieleza mwanamke huy


SERENGETI FIESTA 2014 YAFUNIKA DODOMA,TAZAMA PICHA HAPA

Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo akitumbuiza kwa staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Mo Music akitoa burudani kwa wakzi wa Dodoma waliyofulika kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msanii zao la Serengeti Super Nyota G-Lucky akifanya makamuzi ndani ya uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Y-Tony akiwajibika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa likifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Chipukizi wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince akiwajibika jukwaani.
Msanii zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Kadja Maumivu akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuamkia leo.
Young Killer akimwaga mistari ya Hip Hop kwa mashabiki waliyojitokeza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililokuwa likifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma.
Mr Blue akifanya yake jukwaani.
Recho akiimba jukwaani huku mmoja wa wanenguaji wake akiwajibika kwa staili kali.
Mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes akipagawisha jukwaani.
Vanessa Mdee katikati akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Jux akikamua jukwaani.

DIAMOND AFANYA MAKAMUZI YA NGUVU BIG BROTHER HOTSHOTS



Diamond Platnumz akifanya makamuzi ndani ya Big Brother Hotshots.
STAA wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku huu amefanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi wa shindano la Big Brother Hotshots unaofanyika jijini Johanessburg nchini Afrika Kusini.
Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na watu wawili mrembo Irene 'La Veda' na Idriss. Jumla ya washiriki 26 kutoka mataifa 12 ya Afrika watachuana kwa siku 63 kutafuta mshindi atakayejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 300,000.

BIRTHDAY YA DIAMOND, BEATIFUL ONYINYE WEMA SEPETU AZUA GUMZO!..TAZAMA PICHA NA VIDEO YA KILICHOTOKEA

Stori: Waandishi Wetu
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’.
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Diamond Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya pamoja.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake.
Saa 3:30 USIKU
BUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei.
SAA 4:00 USIKU
BIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh! Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani.
SAA 5:00 USIKU
SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
Nuh Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo.
Risasi Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKU
NGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Wageni waalikwa wakizidi kuingia ukumbini.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki ya Bethidei ya Diamond.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.

Lulu Afunguka Ukaribu Wake na Kadinda..Fuatilia Alichosema Hapa


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefafanua ukaribu wake na Martin Kadinda kwa kudai ni rafiki yake wa karibu na hakuna cha ziada.Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Martin Kadinda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema yeye na Kadinda ni marafiki wa kweli na amekuwa akiinjoi maisha yao kwa kushauriana masuala mbalimbali ya kimaisha tofauti na wengine wanavyojiongeza.Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Kadinda ni mtu wangu wa nguvu hakuna kingine zaidi ya urafiki wa kawaida, manenomaneno ni kawaida kwa wanadamu,” alisema Lulu.

Hii Ndio Zawadi Aliyopewa Diamond Kwenye Birthday Yake, Kwa Taarifa yako Haikutoka Kwa Wema


Jana Ilikuwa Ni Siku ya Kuzaliwa ya Mwanamuziki Anaye Make Headlines Bongo na Nje ya Nchi Diamond Platnumz, Hakika wengi Walisubiri Kuona Mpenzi wake Wema Sepetu Atamzawadia Zawadi gani Kwa Vile Yeye Alizawadiwa gari na Diamond..So Wengi Tulisubiri kuona Atafanya nini ....Lakini Jana Zawadi kubwa iliyotolewa ilikuwa ni Gari Aina la BMW ambalo Diamond Alipewa Zawadi na Management Team yake ..Ikimaanisha kina Babu Tale....Mie Sikuwepo kwenye Party Hiyo kwa anayejua Wema Alitoa zawadi Gani Atujuze Basi Hapo Kwenye Comment.

Kiingereza cha Diamond,The Sporah Show na Kile Cha Shigongo, Straight Talk Africa

Well,inatia moyo kuona waswahili sasa tunaanza kuwa majasiri wa kufanya interview za kiingereza(JAPO BROKEN) na hasa ujasiri huo unapofikia hatua ya kufanya interview katika vipindi vya TV vinavoangaliwa na watu wengi duniani kote.So,jana tar.30/9 nilimsikiliza Diamond akiamua kuwa jasiri na kupima uwezo wake wa kukimudu kimombo pale alipofanya interview ya kimombo na Mrembo Sporah Njau wa The Sporah Show kinachorushwa Clouds TV kutokea London.

Na wakati huu namsikiliza Eric Shigongo akifanya interview na presenter mahiri wa kipindi cha Straight Talk Africa,Prof Chaka Ssali wa The Voice of Africa.Nawapongeza kabisaaaaaa but man,we can still pick a hole or two in the interviews: (1).The guys are trying too hard to impress and to sound relevant,nafikiri wakati mwingine wasipanie au wasiwe na fikra kuwa ndugu zao tunaowaangalia huku tuwakome,i mean wafanye interview wakiwa totally focused on the issues raised in the interviews na wasitake tunaowasikiliza "tuwakome" (2).Sporah alizungumza Queen's English wakati Diamond alitaka watazamaji tuamini kuwa yeye ni Kanye West au 50 Cent.

Hivyo hivyo Eric Shigongo wants us to believe kuwa yeye ni wa mitaa ya Brooklyn New York wakati yeye ni Msukuma through and through....ninachosema,they need not fake their accent,mbona Chaka Ssali ni profesa na anazeekea Marekani lakini hathubutu kusema accent ya kimarekani?

Yeye bado anapiga kiingereza chake cha Kabale Uganda and he's doing good!Nasema hivi,wanastahili pongezi lakini wazungumze kiingereza cha kawaida tu wasitake kutafuna maneno kama kina Obama,kufanya hivyo kunawaboa viewers because for one,they are not fluent,sasa kama hauko fluent utatakaje kujiongelesha accent ya kimarekani,people!Wanigeria na Wakenya mbona wanaongea tu kivyao vyao and we have come to like Nigerian English'oooo,haven't we?

Hongera Diamond,hongera Shigongo,mna afadhali kuliko Mh.Membe,siku moja nilimsikiliza kwenye kipindi kilekile cha Straight Talk Africa niliboreka sana,sikuona tofauti yake na Mulugo

Batuli Afunguka Kuhusu Tetesi ya Yeye Kuvunja Uchumba wa Rose Ndauka


Stori: RHODA JOSIAH
MSANII wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ameshangazwa na madai kuwa, anahusika kuvunjika kwa uchumba wa msanii mwenzake Rose Ndauka na kueleza kuwa hayo ni maneno ya watu wasiomtakia mema.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kufuatia madai hayo, Batuli alisema hajawahi kuwa na uhusiano wowote na bwana wa Rose (Malick) na kwamba ukaribu wao ni wa kikazi tu.

“Jamani siwezi kutoka na mchumba wa Rose kutokana na kwamba ni mtu ambaye namheshimu sana na tumekuwa tukifanya kazi na Rose bila matatizo yoyote. Hizi taarifa zinanishangaza na najua wanaozieneza hawanitakii mema,” alisema Batuli.

Didas Fashion Amshukia Clouds 112 wa Bongo Movies , Asema Amelamba Ndimu na Kufunguka Mazito


Kupitia ukurasa wa Didasfacion wa Instagram Jana , Mwanadada huyu aishie UK ..Amefunguka Makubwa Kuhusu Bongo Movies hususan Muingizaji Clouds 112...Jisomee Mwenyewe Hapo chini:

"Hahahaha @eshasbuheti na wewe umejitoa kwa ajili yangu kama @stevenyerere2 au?. Mungu huyu analipa hapa duniani. ... Nina mengi ya kuongea alafu mie huwa siongei kwa maneno naongea na evidence. Nina dhambi za mtu natembea nazo na siku kichaa kikinipanda nitazimwaga hadharani, watu wataacha midomo wazi. Watu wanavaa majoho ya mungu kujifanya wema. Na hapo ndio mtajua kwanini movie yangu ya Mateso Yangu Ughaibuni sijaitoa mpaka leo. Nilinyamaza, ila subirini ma evidence yanakuja. Mi mstaarabu ila ni Kiazi kibovu mnooo.

Nasema nimeramba ndimu, nimechoka sasa ni wakati wa kutapika, naomba waandishi wa habari msogee huku kwa page yangu haraka. Maana ule muda muwafaka umekaribia. Mimi ni Mmanyema halisi. Nimekaa kimya nimechoka. Hawa ni wanawake wenzangu. Pole sana @sabrinarupia alafu ninavyo kupenda wewe dada acha tu. It's time.

Jamani mnamuona huyu kaka hapa? Huyu kaka anaitwa Frank kwa wale msio mjua. Huyu kaka ndio alikuwa aje UK kucheza movie ya MATESO YANGU UGHAIBUNI. Na tulisha kubaliana hadi bei maskini na kila kitu kilikuwa poa. Mara ghafla nikapokea simu ya kinafki, na wakati huo mie nilikuwa sijui lolote kuhusu bongo movie. Nikaambiwa huyu kaka ninae taka kumchukua hajui kucheza wala ku direct movie. Nika pampiwa vibaya mnoo mpaka nikatia akili. Frank kokote ulipo naomba unisamehe najua ulikuwa tayari umekuwa na tamaa ya safari ya kuja ulaya, ila waziba rizki wakafanya yao. Wacha naishi hapo. Hii ni intro tu. Hadithi kamili inakuja. Kaeni na ndimu zenu.
-----------------------------------
Clouds 112 Haya uliniita mimi tapeli tena mzulumati, nimekudhulumu million 8 za kuja kucheza movie, ukaenda mpaka kwenye magazeti kusema, nikapigiwa na wenye magazeti, nikawapa ukweli na ushahidi. Tena huu ni mfano tu, ninazo nyingi na za aibu, na bado naendelea. Frank aliniomba nimlipe Tsh 2 million kucheza hiyo movie, nikakubali, wewe ukasema kila kitu utafanya bure ila nikisha uza movie nikufikirie, sasa leo umemfanya @stevenyerere2 kajiuzulu eti kisa kanisaidia uzinduzi, na hela ya PSPF tumekula, huu ni mfano nakuja kumwaga mengi. Ulijitole kila kitu bure uje ulaya, leo umenipaka mavi dunia nzima mimi tapeli, unawafanyia fitna watu wote wanao kaa karibu na mimi. Hii ni haki? Sawa mimi tapeli dhulumati, zote ni njia za kutafuta riziki. Tutafika hata mahakamani. Bado na rudi na mazito zaidi. Ongezeni ndimu


Clouds 112 Nilihangaika kwa nguvu zangu ili nifanye kitu tofauti. Nahangaika na familia yangu. Hata kama movie niliicheza kimaskini, kwani nyie movie zenu mnazicheza kitajiri? Nimeiba, nimenyang'anya, nimekopa kukupandisheni ndege kuja kucheza movie. Kuna matajiri wangapi wana hela zao na visa kupata hawapati? Wangapi wanaingia ubalozini wanakosa visa. Eti unaaenda kumwambia distributors wasichukue movie yangu kisa umedhulumiwa. Unaweza wewe kuzilipa gharama zangu hata kama ni ndogo? Rizki yangu ninavyo itafuta unaijua? Ninavyo hangaika kutafuta maisha na kupigana usiku na mchana unajua? Hujaziba bado rizki yangu ya hiyo movie, mungu akiniandikia hata Kenya watanunua na wata distribute, karoge sasa. Am sick and tired. Nime nyamaza ila nimeshindwa kuvumilia. Wapenzi wangu naomba mnisamehe. Nahangaika kutafuta riziki nile kwa jasho langu na nguvu yangu. Sijakutuma unipe offer yakucheza movie bure ili ukalalamike. Sijamaliza evidence. Mpaka za mapenzi pia. Nakuja nazo

Nadhani Kuna haja ya Kusikia Kutoka Upande wa Pili wa Clouds 112...

Dada wa Diamond Esma Atoa Mipasho Kupitia Instagram Wiki Mbili tu Baada ya Kuolewa

Dada wa Mwanamuziki Diamond Anayejiita Esma Plainum Ambae Ameolewa Hivi Karibuni na Petit Man Amepost Video Kwenye Instagram Page yake Huku Akitoa Mipasho ya Taarabu yenye Kuwananga Wanao Ona Wivu Juu Yake Kuolewa...Baadhi ya Maneno yanasikika Akiimba
'Mwaona Donge la Nini Kama Mnaweza Pandani Juu mkazibe'

Je Kunani Tena ? 

Jionee Mwenyewe Hapa:
((bofya hapa))

HIZI NDIZO PICHA ZA AWALI ZA KILICHOJIRI KWENYE BIRTHDAY YA DIAMOND - ZIANGALIE HAPA









AIBU! MKE, MUME WAZICHAPA WAFUNGA MTAA

Hii ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu,  Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.
Timbwili zito likianza kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata.
Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
Mke akimlia 'taimingi' kumbwaga mume wake kwa mweleka.
MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
Mara Puuuuu...!! wote chini
“Sasa akiwa pale baa, alizidi kunogewa na masaa yalizidi kupotea ndipo Zeno alirudi nyumbani na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo huku akisikia harufu kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,” kilidai chanzo hicho.
Mume (Bw Zeno) akimburuta mkewe kwa ghadhabu.
AMUIBUKIA BAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia ‘kunyonya’ kilevi kikali.
ZACHAPWA
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya kuzidiwa na kilaji.
Wote wakichukua uamuzi wa kuzima timbwili hilo.
LAHAMIA NJE YA BAA
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
Mke(Bi Mwajuma Mtata) akijaribu kuzuia kupigwa picha na kamera za wanahabari.
WARUDI NYUMBANI
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
Jirani akihoji kulikoni mpaka iwe hivi...
ETI WAMEYAMALIZA!
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX