Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » ASKARI WATATU WAJERUHIWA KWA MLIPUKO WA BOMU SONGEA

ASKARI WATATU WAJERUHIWA KWA MLIPUKO WA BOMU SONGEA

Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi

Eneo la tukio likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao.
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini

ASKARI watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.

Tukio hilo limetokea September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja laMatarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu waliokuwa doria.

Askari hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu. Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendohicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitiavyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX