Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label picha. Show all posts
Showing posts with label picha. Show all posts

SERENGETI FIESTA 2014 YAFUNIKA DODOMA,TAZAMA PICHA HAPA

Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo akitumbuiza kwa staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Mo Music akitoa burudani kwa wakzi wa Dodoma waliyofulika kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msanii zao la Serengeti Super Nyota G-Lucky akifanya makamuzi ndani ya uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Y-Tony akiwajibika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa likifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Chipukizi wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince akiwajibika jukwaani.
Msanii zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Kadja Maumivu akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuamkia leo.
Young Killer akimwaga mistari ya Hip Hop kwa mashabiki waliyojitokeza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililokuwa likifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma.
Mr Blue akifanya yake jukwaani.
Recho akiimba jukwaani huku mmoja wa wanenguaji wake akiwajibika kwa staili kali.
Mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes akipagawisha jukwaani.
Vanessa Mdee katikati akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Jux akikamua jukwaani.

BIRTHDAY YA DIAMOND, BEATIFUL ONYINYE WEMA SEPETU AZUA GUMZO!..TAZAMA PICHA NA VIDEO YA KILICHOTOKEA

Stori: Waandishi Wetu
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’.
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Diamond Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya pamoja.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake.
Saa 3:30 USIKU
BUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei.
SAA 4:00 USIKU
BIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh! Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani.
SAA 5:00 USIKU
SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
Nuh Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo.
Risasi Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKU
NGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Wageni waalikwa wakizidi kuingia ukumbini.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki ya Bethidei ya Diamond.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.

MAJANGA:PAKA AFUNGWA HIRIZI MTINI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo, Morogoro.
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.
Baadhi ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji Mpya.
Watoto wakishudia tukio hilo la kushangaza.
“Tulifika hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa bado kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa kupiga kelele mfululizo.
“Tuliposogelea tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi. Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.
“Unajua eneo hili lina miti mingi lakini wahusika wamekuja kumpigilia misumari paka huyu hapa. Mimi nasema wasakwe hawa watu tuwajue,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Said.
Umati wa watu wakishudia tukio hilo linalohusishwa na ushirkina.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya msikiti huo, Haji Said Dihole alipohojiwa na mwanahabari wetu alisema:
”Kama kuna mtu alitaka kutujaribu angemuweka paka huyo kwenye eneo letu la msikiti angeipata habari yake, pia nasikia tukio kama hili liko kwa majirani wetu pale Kanisa la T.A.G Mwembesongo, nenda kashuhudie.”
Paka huyo baada ya kutolewa mtini.
Baaada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of  God ‘T.A.G’ linalofahamika kwa jina la Bethel Revival Temple lililopo Mwembesongo.

Skirt Fupi Maofisini Zinapunguza Ufanisi wa Kazi kwa Wanaume


Moja kwa moja nianze kuwaomba dada zangu ambao wanatuvalia vimini ofisini punguzeni au acheni jamani wengine tuna mioyo ya udongo kwa sababu mnapofanya kazi na sisi halafu karibia mapaja yote yapo nje jamani mnatufanya tufanye kazi ambazo hazina ufanisi maana mnatunyima concentration jamani vaeni basi sketi ndefu au kusema sketi fupi inaendana na mambo ya ofisini.
Jamani acheni wengine jamani tuna mioyo ya petroli.

JAMANI AGNESS MASOGANGE NI SHIIIIIIIIIIIIDA,CHEKI TOTO LILIVYOUMBIKA




Faida Ama Uzuri wa Kuoa Single Mothers na Wadada Over 35 years


Ndoa nyingi zina changamoto lakini nimegundua ukioa single mother au dada ambae ni 35+ hawa watu mara nyingi huwa ni wife materials ukilinganisha na hawa wenye age ya 20-35.

*Hawa watu wana commitment sana katika ndoa zao.
*Wanakuwa washapitia changamoto nyingi zinazohusisha mahusiano so huwa hawasumbui.
*Wengi wamekomaa kiakili na wanajua jinsi ya kuhandle mume na familia kwa ujumla
wana mazuri mengi.

Kama hujaoa ukipata watu wa namna hii usipoteze fursa

MREMBO HAMISA MABETO AMUANIKA MCHUMBA WAKE

MAHABA niue! Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii  huku akimmwagia sifa kemkem.
Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya, Hamisa alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon!
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.
Mtoto mzuuuuri... kunako fani ya mitindo Bongo, Hamisa Mabeto akipozi.
“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.

Style Zingine za Nguo Ni Shida Tupu, Embo Ona Alichovaa Jokate Hapa

Style Zingine za Nguo Ni Shida Tupu, Embo Ona Alichovaa Jokate Hapa, Kapendeza or Not ?

HOT PHOTO:- JOKATE MWEGELO ATOKELEZEA KIHIVI





SEMA NENO MOJA KWENYE HILI VAZI

Siku hizi kumekuwa na mavazi ya kila aina yanavaliwa na madada zetu, sasa kwa vazi hili je unaona yupo sahihi?

WOLPER AMESHARE NASI PICHA HIZI TAMUU



PICHA KALI ZA MTOTO RISPER FAITH KUTOKA KENYA


 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX