Wananchi wakisaidiana kuokoa mali za Msikiti wa Mtambani mara baada ya kushika moto uliowahi kuzimwa.
Kikosi cha zimamoto kikiwa eneo la tukio kutoa msaada.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa eneo hilo la tukio.
(PICHA ZOTE NA DAR ES SALAAM YETU BLOG)
(Picha hii ni wakati msikiti huo ulipoungua mara ya kwanza Agosti 13, mwaka huu)
MSIKITI wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam umeungua tena kwa moto leo mchana. Hii ni mara ya pili msikiti huo kuungua kwa moto baada ya ile ya awali ya Agosti 13 mwaka huu. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.









Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida. 

Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni. DEREVA wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.