Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label matukio. Show all posts
Showing posts with label matukio. Show all posts

Uzuri Wamponza Dada Huyu, Wenzake Wamuonea Wivu na Kumrarua Sura

WASICHANA ndugu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 na 18 wamemshambulia kwa visu binti mwenye miaka 15, kwa lengo la kumkomesha kwa sababu anasifiwa kuwa mzuri. 

Katika tukio hilo la aina yake, ndugu hao walimvizia msichana huyo, Julia Alvarez(15), njiani wakati anakwenda nyumbani mjini Juan Domingo Peron kwenye jimbo la Formosa Kaskazini mwa Argentina.

Kwa mujibu wa kauli za wasichana hao, walifanya unyama huo kwa kuwa hawakupenda kusikia sifa alizokuwa anapewa binti huyo kuwa ni mrembo sana.

Mwathirika huyo, Alvarez alisema wakati anashambuliwa, wasichana hao walisema, walitaka kumharibu awe anatisha kama mcheza sinema za kutisha, Chucky.

Msichana huyo alisema alivamiwa wakati anakwenda nyumbani kujiandaa kwenda kuwatembelea rafiki zake, wasichana wawili walimvamia, wakaanza kumpiga na kumwangusha chini. Alvarez amesema, baada ya yeye kuanguka, wasichana hao walitoa visu na wakasema,

“Kila mtu anasema una mvuto, tukikumaliza mvuto wote utaisha, watu watakuita Chucky”. Mtoto huyo alikatwa kwa visu kwenye sehemu mbalimbali mwilini hasa usoni na mgongoni. Baada ya kumuumiza binti huyo, wasichana hao walikimbia na kumwacha amelala kwenye dimbwi la damu, mpita njia alimwona, akamkimbiza hospitali.
Inadaiwa kuwa, awali polisi hawakuchunguza tukio hilo lakini dada wa majeruhi aliweka picha za mdogo wake kwenye mtandao wa facebook, ndipo watu wakashinikiza haki itendeke. Wasichana waliomshambulia Alvarez wakamatwe.

“Walimwonea wivu mdogo wangu kwa muda mrefu, na kila mara walimkashifu na kumtukana lakini hatukutarajia kufika mbali kiasi hiki. Nimejaribu kuwa mvumilivu kwa ajili ya mdogo wangu mrembo lakini kila mara nikimwona nataka kutokwa machozi, wameharibu maisha yake,” amesema mwanamke kwenye ukurasa wa facebook akijitambulisha kuwa ni dada wa binti aliyejeruhiwa.

“Alisema anataka kujiua kwa sababu sasa akijitazama kwenye kioo anajiona mbaya, imeharibu familia yetu,” alieleza mwanamke huy


MAMA WEMA USIJISAU, WEWE NI MTU MZIMA!MAMA WEMA


HII ni mara ya pili ninaandika kuhusu Miriam Sepetu, mama mzazi wa muigizaji nyota, Wema Sepetu. Bado ninakumbuka vizuri nilichokiandika mara ya kwanza, ilikuwa ni kuhusu tabia yake wakati ule. Alipenda sana kuzungumza na magazeti kuhusu nyenendo za mwanaye katika uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond.
Ingawa ni kweli mzazi ana nafasi muhimu katika maisha ya kimapenzi ya mtoto wake, lakini siyo jambo la busara kuingilia kupita kiasi kama yeye alivyokuwa akifanya wakati ule, maana ilikuwa ni kama yeye ndiye mhusika mkuu.
Ninachoshukuru ni kwamba baadaye alijirudi, akaacha kumsakama Diamond, akakubali maisha yao ni yao na sasa vijana wanatumia vizuri fursa waliyonayo katika ulimwengu wao wa mapenzi. Kwa jinsi wanavyokwenda hivi sasa, halitakuwa jambo la ajabu kama wataishia kufunga ndoa, ingawa historia haiongei vizuri kuhusu ndoa za mastaa, hasa wa Kibongo!
Leo ninazungumza naye kwa mara nyingine, nikiwa na imani kuwa kama ilivyotokea awali, atayafanyia kazi nitakayomweleza. Jumapili iliyopita, Wema Sepetu alifanya sherehe ya kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa, akitimiza umri wa miaka 26, tokea atoke tumboni mwa Miriam.
Sherehe ilifanyika nyumbani kwake binti, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marafiki pamoja na ndugu wa karibu. Kwa mujibu wa waliokuwepo, ilikuwa ni bonge moja la shoo kuwahi kutokea, kwani licha ya msichana huyo kupewa zawadi ya magari mawili, pia watu walikunywa, wakala na kusaza!
Lakini wakati mama alipopewa nafasi ya kuzungumza chochote, kwa namna ya kushangaza, alianza kuzungumza maneno yasiyofaa kutamkwa na mzazi, yakiwemo matusi dhidi ya Kajala Masanja, muigizaji mwingine ambaye siku hizi ni kama paka na panya na Wema.
Wema na Kajala walikuwa ni marafiki wakubwa na kila mmoja anatambua kuhusu hili. Baadaye katika hali ambayo haikutarajiwa, wakakosana na kuleta uhasama mkubwa kati yao.
Mama alitamka matusi ya aibu kwa Kajala. Ni sawa, ana uchungu na mwanaye, lakini hivi ni kweli uchungu huo unaweza kupoteza busara za mama mtu mzima kuzungumza maneno ya ovyo hadharani?
Katika hali ya kawaida, mama yetu huyu alistahili kutumia nafasi ile kutoa ushauri kwa mwanaye kujiweka mbali na mabifu dhidi ya marafiki zake, tena angeweza kumsihi kufikiria kurejesha urafiki wake kwa Kajala, hata kama ni kinafiki!
Lakini leo yeye anashadadia ugomvi wa watoto, hivi hajui hawa vijana wa sasa hawaeleweki? Itakuwaje hawa masistaduu wakirejesha urafiki wao?
Binafsi naamini hakuna rafiki wala adui wa kudumu katika maisha, kitu cha msingi ni kuwa mwangalifu wa kauli wakati wa mgogoro na kutojianika sana kwenye urafiki. Wema na Kajala ni marafiki watarajiwa, hasa kwa sanaa wanayoifanya!
Mama Sepetu ni mwakilishi wa wazazi, sasa anataka baba na mama zetu nao kwenye shughuli zetu watumie nafasi hizo kuwatukana tuliokosana nao sisi katika maisha yetu ya ujana?
Mama hapa amepotoka na nimshauri tu amuombe radhi Kajala. Matusi haya yanasambaa kwa kasi katika mitandao na simu za mikononi. Natambua wanafahamiana vizuri tu kwa sababu aliishi naye kama mwanaye wakati wa urafiki wao na Wema.
Amtafute na ampigie magoti kwa nia njema kabisa. Hawezi kuonekana mjinga kwa sababu moja ya vitu vinavyompa mtu heshima ni uwezo wake wa kutambua makosa na kuwa tayari kukiri. Asipofanya hivi, kwa sababu zozote, atadharaulika, lakini akiomba radhi, ataonekana muungwana. Ni juu yake kuamua anavyotaka tumuone!

SOMA ALICHOKIANDIKA MASANJA MKANDAMIZAJI BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ KUMZAWADIA WEMA SEPETU GARI


BMW LA WEMA UTATA MTUPU

Achana na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya ‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa ndani ya Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa na meneja wake.
NYUMBANI KWA MADAM
Pati hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Katika shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina, walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.
NISSAN MURANO
Akiwa Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.
Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo Mumy...tafadhali pokea hicho kidogo hiki nilichojaliwa leo.”
BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.
Martin Kadinda akionyesha funguo ya Gari aina ya BMW aliyomzawadia Wema.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni mingi.
Baada ya kuona hivyo, Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.
MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.
Muonekano wa keki ya ‘bethidei’ ya Wema.
Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata, kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram akaandika:
“....Gari hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao....”
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akimlisha keki mama yake.
MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”
MASWALI
Huku Kadinda akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa mastaa walioalikwa (jina kapuni).
Akimlisha keki mamamkwe wake.
MENGINE YATOKANAYO
Pati hiyo ya Wema iligawanyika mara mbili ambapo ya kwanza ilianza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 huku nyingine iliyohusisha watu maarufu ikianza baadaye hadi ‘kokoriko’.
KEKI 69 MEZANI
Katika hali isiyo ya kawaida, sherehe hiyo ilikuwa na keki zipatazo 69 ambazo zililetwa na baadhi ya mastaa ambao walihudhuria sherehe hiyo huku kukiwa na vinywaji vya kufa mtu (wiski tu), loko bia tupa kule.
Akimlisha keki Jokate.
NDAFU
Kwa upande wa nyama kulikuwa ndafu mzima ambaye watu walimtafuta hadi wakasaza.

MAMA DIAMOND AMTANGAZA RASMI MKWEWE  
Katika sherehe hiyo, mama Diamond alipopewa kipaza sauti ‘maiki’ ili anene chochote alisema kuwa Wema ni mkwe wake wa halali na kwamba anampenda hivyo asiwe na wasiwasi kwani hakuna mkwe mwingine atayatokea zaidi yake.
Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akifungua shampeni kwaajili ya shughuli hiyo.
“Jamani huyu ndiye mkwe wangu, Mrs Chibu (Diamond) ndiye mkwe wangu hasaaa...,” alisema mama Chibu huku watu wakishangilia.
MILIONI 10
Kwa mujibu wa Kadinda, shughuli hiyo iligharimu zaidi ya Sh. milioni 10 hadi kukamilika na kuonekana ya tofauti na pati nyingine za mastaa Bongo.
Wema akiongea jambo kabla ya kukata Ndafu.
AMWAGIWA NOTI
Ulipofika muda wa kutunzwa zawadi, watu walijitokeza kumtunza Wema fedha ambazo hazikuweza kupatikana kiasi chake mara moja huku staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiweka rekodi kwa kumwaga ‘minoti’ mingi katika hafla hiyo.

Tabia za Wasichana wa Tanzania Kulingana na Makabila Yao


1.WASUKUMA:
Hawa ni madem tuseme tu blackbeauty yaani mademu wana ngozi smooth ya kupendeza sana lakini niweusi kama mkaa but mimi huwapendea one thing. Demu msukuma akikupenda amekupenda for real ("Eti" walivyo mabwegge washaanza kusmile aaaiii..!) Hawa ni mademu hawapendi usafi, sufuria ya kupika chakula ndio wanaoshea nguo ndio wanaogea .na pia kufulia chupi zao. Figure ni nzuri sana sauti poa kama ya rihana lakini tabia ni mbovu.

2.WARANGI
Hawa ni mademu wengine wasupuu sana yaani hawa ndio mungu alicopy paste the real image yake akawapa yaani mademu wameiva poa, rangi ya mzungu figure nzuri lakini ni wafupi, shida moja tu, wao ni washamba sana wamelogewa kazi za bar.

3.WABENA
Mademu wana sura middle body, figure nzuri lakini ngozi ngumu kama ya ngamia shida ingine ni kuiga iga kama wachina ushamba nao ni asili yao asipofanya kazi ya ndani kwake maisha ni bado.

4.WACHAGA
Hawa ni madem wanajua maisha ni nini yaani madem wako na bidii sana lakini shida ni wezi!!! sura wako poa sana,body figure aina shape yaani yao wengi ni flat screen na pia ziko shapeless.

5.WANYAKYUSA
Hawa ni mademu wana tabia nzuri yaani mademu watulivu but shida ni sura aipo sura haiko, body na figure iko D ni watu wako hardworking sana ushamba pia upo kwa wingi hupenda Kujivunia kuwa washamba.

6.WAZARAMO
Tunajua nyinyi mnajua kupika poa sana, watoto wazuri wameiva lakini matusi yanashinda akili zenu na uvivu yaani demu ameiva lakini akikutusi unafeel tu kumlima makofi kazi yao kubwa kupaka rangi kucha.

7.WAZIGUA
Mademu wasupuu kama mtoto wa Kagame figure poa lakini shida ni kimbelembele na makelele sjui ni nani aliwafunza kulia kisanii kwenye misiba pia mna hasira za kishenzi na utoto mwingi na kujiona eti mnajuuuwa, kumbe hewa tu.

Asante na matusi nishazoea ila ukweli tutawaeleza tu.

SERENGETI BOY ANASWA NA MKE WA KIGOGO LIVE AKIVUNJA AMRI YA SITA

KABAANG! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.
Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo.
Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka.
“Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Akisainishwa kulipishwa faini.
“Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.
Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa pesa hizo.Barua ya makubaliano ya kulipwa pesa kwa kigogo huyo shilingi laki tano.
Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya makubaliano jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na iwe kama fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu.
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na kudai ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu.
Mke huyo wa Kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Mwanaidi akiwa analia akiomba msamaha kwa mumewe.
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya kwani ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi wa mtaa huu nitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi za kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.

Je Unaipenda Facebook ? Mtandao Pinzani Umezinduliwa , Waja kwa Kasi ya Ajabu


Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.

TBS YAONYA WANANCHI WANAO VAA NGUO ZA NDANI (CH**PI) ZA MITUMBA

Shirika la Viwango (TBS) limewataka wananchi kutonunua nguo za ndani za mtumba ili kuua soko la bidhaa hizo zenye athari kiafya.

Kaimu mkurugenzi anayehusika na udhibiti ubora wa TBS, Mary Meela alisema nguo hizo ni hatari kwani zinaweza kueneza magonjwa mbalimbali hasa ya ngozi.


Alisema lengo la ombi hilo ni kukomesha uuzaji wa nguo hizo ambazo zinaweza kusababisha maambukizi kutoka kwa aliyekuwa anavaa nguo hiyo kwenda kwa mtu wa pili.
chupi

Meela alisema shirika lake linashindwa kukomesha biashara hiyo kwa sababu halijapewa nguvu za kisheria kukataza watu kufanya biashara hiyo kama ilivyo Zanzibar, hivyo amewataka wananchi kutambua madhara hayo na kuacha kununua.
“Nguo za ndani zina bei ndogo hata mtu wa chini anaweza kumudu. Sioni sababu ya mtu kwenda kununua za mtumba,” alisema.

Wema Sepetu 'Watu Wenye Majungu Hawanisumbui Kichwa Kabisa Nabaki Nawatazama Tu'


Stori: Mayasa Mariwata
MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi.

Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.

“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Sugu amwagana na Mke wake…Mwanamke Afunguka Mazito




Mwigizaji wa filamu nchini FaizaAlly amemwagana na mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu …

Kupiia Instagram, Faiza ameandika maneno yanayoonyesha amemwagana na Mh.Sugu ambaye pia ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema.

Skirt Fupi Maofisini Zinapunguza Ufanisi wa Kazi kwa Wanaume


Moja kwa moja nianze kuwaomba dada zangu ambao wanatuvalia vimini ofisini punguzeni au acheni jamani wengine tuna mioyo ya udongo kwa sababu mnapofanya kazi na sisi halafu karibia mapaja yote yapo nje jamani mnatufanya tufanye kazi ambazo hazina ufanisi maana mnatunyima concentration jamani vaeni basi sketi ndefu au kusema sketi fupi inaendana na mambo ya ofisini.
Jamani acheni wengine jamani tuna mioyo ya petroli.

LAANAAA..!!PATI YA ANTI LULU MASHOGA KIBAO!

Makubwa! Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ ameangusha bonge la pati huku ikihudhuriwa na mashoga kibao.
Wanaume 'tata' wakilishana keki katika sherehe ya bethidei.
Pati hiyo ya kufuru ambayo ilikuwa ni ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya kijana wa mjini aliyetajwa kwa jina moja la Abdul iliyoandaliwa na Anti Lulu ilifanyika katika Hoteli ya KB iliyopo Kijitonyama, Dar, wikiendi iliyopita ambapo ilihudhuriwa na watu mbalimbali lakini asilimia kubwa ya waalikwa walikuwa ni ‘wanaume tata’.
Aunty Lulu akikata mauno kwa raha zake.
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzama ndani ‘kimafia’ ambapo lilimshuhudia Anti Lulu akikata mauno ya kufa mtu baada ya kusikia kibao kata kilichokuwepo hotelini hapo.
Wageni waalikwa wakiendelea kujiachia katika bethidei hiyo.
Katika pati hiyo wanawake wengi walionekana wakiwa nusu utupu na wengine baada ya kuingia walivua nguo na kuvaa vichupi na braa kisha kuzama kwenye bwawa la kuogelea wakifuatiwa na mashoga hao waliokuwa wamevalia boksa na singlendi.

WEMA, DIAMOND WANADAIWA KUFANYIANA 'TIMINGI' YA KUMWAGANA!

Diamond..Mh! Upepo mbaya unaivumia kapo ya mafahari wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo wanadaiwa kufanyiana ‘taimingi’ ya kumwagana, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu makini, wawili hao wamepotezeana kwa muda mrefu huku kila mmoja akifanya yake lakini kila mmoja anashindwa kujitoa mhanga na kusema hawapo pamoja akihofia kuonekana ndiye tatizo.
“Kifupi ni kwamba Wema na Diamond hawapo pamoja kwa kipindi kirefu, yawezekana wanawasiliana lakini si kwa mapenzi labda kwa mambo mengine. Diamond anazuga kama yuko kwenye shoo, hata akirudi Bongo hawana ukaribu na Wema kama ilivyokuwa zamani, anazuga kidogo kisha anaondoka tena.
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinum.
“Wema naye hivyohivyo, yupo bize na mambo yake, inasemekana yupo na kigogo f’lani hivi Mkongomani ndiye anampa jeuri mjini kama ulivyoona juzikati amemwaga mapesa ukumbini.
“Inasemekana Mkongomani huyo amemfungulia pia ofisi mpya ya kurekodia filamu pamoja na kumnunulia gari jipya,” kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, Jumapili (jana) Wema alipanga kutangaza rasmi kumwagana na Diamond wakati alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na kumtangaza mwanaume wake mpya.
“Jumapili (jana) ndiyo kila kitu kitakuwa hadharani maana Wema amepanga kutangaza hadharani kwenye bethidei yake,” kilizidi kudai chanzo hicho.
Diamond na Wema wakila ujana.
Mwanahabari wetu alipokutana na Wema nyumbani kwake na kumuuliza kuhusu madai hayo aliyakanusha yote lakini akawa mzito kidogo katika suala la kutoonana muda mrefu na Diamond.
“Madai yote hayo siyajui! Nina bwana mpya? Eti kaninunulia gari! Amenifungulia ofisi! Sijui nimeachana na Diamond! Hayana ukweli wowote,” alisema Wema kwa mshangao mkubwa.

MSHIRIKI WA MISS TANZANIA HUSNA MAULID AKUTWA LIVE KITANDANI NA MODEL MAARUFU

KABAANG! Miss Sinza 2001 na aliyekuwa pia mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid amenaswa akiwa kimalovee laivu kitandani na modo maarufu Bongo aliyejulikana kwa jina moja la Calisa.
Miss Sinza 2001, Husna Maulid akila ujana na modo maarufu Bongo anayejulikana kwa jina moja la Calisa.Picha hizo ambazo zinamuonesha Husna na Calisa wakiwa wamekumbatiana zimevuja kiitelejensia na kumfikia paparazi wetu kisha akawauliza kulikoni?  Ni wapenzi?
Modo, Calisa
“Siyo kweli sina uhusiano na Calisa, sina boyfriend na sitaki mwanaume kwa sasa, Calisa ni rafiki yangu tu,” alijibu Husna huku Calisa akijibu:
Husna Maulid.
“He hebu ngoja kwanza nitakupigia, hizo picha kaleta nani?”

Je Wajua..!!! Masanja Mkandamizaji Amzidi Utajiri Diamond Platnums


Wadau,
Hii kitu nimeisikia Clouds FM kwenye kipindi cha Gospel Trucks na Harris Kapiga!
Naomba kufahamu zaidi huyu mpendwa uwekezaji wake unakua kiasi gani na anatumia mbinu zipi kukuza kipato chake ili vijana tujifunze kutoka kwa vijana wenzetu. Nilifahamu ana kipato kizuri lakini amekuaje kiasi cha kumzidi Diamond? Mungu amkbarikie zaidi
Asante

Wema Sepetu Amsaka Meninah Kwa Kumkwapulia Diamond

Habari mpya zinasema kuwa Wema Sepetu anamsaka meninah kwa udi na uvumba sababu ikidaiwa ni Meninah kutoka kimapenzi na Diamond kwa siri kubwa huku Wema akiwa hana hili wala lile mpaka mapenzi ya wawili hao yalipoanza kukomaa na kuchanua nje na watu kujua.

Wema Sepetu
Inadaiwa kuwa Meninah tayari pia amejua kuwa anasakwa na Wema hivyo kuingiwa na hofu, ingawa akizungumza na gazeti moja la

udaku juzi Meninah alisema kuwa hatoki na Diamond bali anasingiziwa tu.
menina

Kilichomtokea huyu simba wakati akijaribu kumla Kiboko, jionee mwenyewe tu [video]


Mnyama anapokufa, vitu vilivyopo tumboni huwa vya kwanza kuanza kuoza na kusababisha mkusanyiko wa gesi. Wingi wa gesi hiyo mara nyingi husababisha mzoga kuvimba, kama gesi haina njia ya kutoka nje. Mpasuko wa mzoga huo husababisha “mlipuko” kutokana na shinikizo (pressure) linalosababishwa na mkusanyiko wa gesi. Na hicho ndio kilichotokea wakati Simba huyu akijaribu kula mzoga wa kiboko.

Simu za iphone 6 Kimenuka, Watumiaji wa Simu Hizo Walalamika Zinapinda


Watafiti wamechanganyikiwa kuhusu ikiwa kampuni ya Apple inapaswa kutoa kauli yake kuhusu ripoti kuwa simu yake mpya ya iPhone 6 inajipinda mtumiaji anapoishi kuiweka ndani ya mfuko wa suruale yake.
Watu kadhaa ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao kwenye mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa na tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa 'Geek.com' pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.

Hackers watishia kuvujisha picha za utupu za muigizaji wa Harry Porter Emma Watson kufuatia hotuba yake ya UN

Staa wa filamu ya ‘Harry Potter’, Emma Watson alitoa hotuba kwenye Umoja wa Mataifa kuwataka wanaume kuungana katika harakati za usawa wa kijinsia. Hackers wametishia kuvujisha picha za utupu za mrembo huyo ambaye ameamua kujitolea kutetea haki za wanawake.
Sony Ericsson Empire Film Awards: Winners Boards
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, mtandao wa 4chan ambao umevujisha picha za mastaa kibao wa Marekani siku chache zilizopita umeweka tangazo lenye picha ya muigizaji huyo na kudai kuwa picha zake zitaingia mtandaoni siku nne zijazo.
Mtu aliyeweka post hiyo ameandika: Watson makes stupid feminist speeches at UN, and now her nudes will be online, HAHAHAHAHAHAHAH,” claiming that it is really going to happen. Feminist bi**h was going to show the world she was as much of a wh**e as any woman.”
Hadi sasa picha za mastaa mbalimbali wakiwemo Kim Kardashian, Rihanna na wengine zimevuja.
Itazame hotuba hiyo hapa.


ALIYEUA MKE KWA WIVU WA MAPENZI NAYE AUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI


WATU wenye hasira wamempiga hadi kumuua mwanamume, aliyemuua mke wake kwa kumpiga rungu tumboni.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, alisema tukio hilo la Septemba 20, mwaka huu katika Kijiji cha Mzogole wilayani Mpwapwa, ambapo mtu mmoja, Mwajuma Chomola (48) aliuawa kwa kupigwa na rungu tumboni upande wa kushoto na mume wake, Richard Kodi (55).

Hata hivyo, alisema Kodi naye aliuawa Septemba 21, mwaka huu baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi. Alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.

Aliuawa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo, amekufa baada ya kupigwa na mtu huyo.

Misime alisema uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.

Kamanda huyo alisema Kodi alimuua mkewe huyo, aliyekuwa akiishi naye baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe, iliyokuwa kijijini hapo, akidhani kuwa alikuwa ameenda kwenye masuala mengine.
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX