Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label msaada. Show all posts
Showing posts with label msaada. Show all posts

Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya


Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini. 
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee

Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga 0 Mapenzi Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita. Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu. Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili. Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake. Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope. Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua. Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia kumuoa. Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya magonjwa. Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7. Facebook kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber anatumiwa mioyo na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali. Nahisi kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit, ila bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto naye. Yaani sijui nifanyeje, nimbwage. Naona sio waifu matirio. Ataniua jamani.

Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita.

Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu.

Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili.

Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake. 

Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope.

Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua.

Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia kumuoa.

Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya magonjwa.

Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7. 

Facebook kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber anatumiwa mioyo na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali.

Nahisi kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit, ila bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto naye. 

Yaani sijui nifanyeje, nimbwage.

Naona sio waifu matirio.

Ataniua jamani.

MREMBO HUYU ANAOMBA MSAADA WA MILLION TANO KWA AJILI YA MATIBABU

Msichana Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75.

Uvimbe huo unaomfanya alie kila mara uliifanya Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha DTV, kuwasiliana na daktari aitwaye Sabapathy wa India, aliyekubali kuifanya kazi hiyo kwa kiwango hicho cha fedha, tofauti na madai ya awali kuwa zingehitajika shilingi milioni 30.
Daktari huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo kama hayo ambaye hali yake inaendelea vyema, alisema msichana huyo atarejea katika hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini kwake na kumpangia kwa ajili ya upasuaji hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Zuhura amewaomba Watanzania kumsaidie ili kuweza kupata matatibu hayo aweze kupona na kuendelea kuwalea watoto wake ambao ni wadogo wanaohitaji msaada wake kama mama na kwamba aliyeguswa na tatizo linalomkabili anaweza kumsaidia kupitia simu yake ya mkononi namba 0717319555.
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX