Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label bongomovie. Show all posts
Showing posts with label bongomovie. Show all posts

Lulu Afunguka Ukaribu Wake na Kadinda..Fuatilia Alichosema Hapa


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefafanua ukaribu wake na Martin Kadinda kwa kudai ni rafiki yake wa karibu na hakuna cha ziada.Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Martin Kadinda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema yeye na Kadinda ni marafiki wa kweli na amekuwa akiinjoi maisha yao kwa kushauriana masuala mbalimbali ya kimaisha tofauti na wengine wanavyojiongeza.Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Kadinda ni mtu wangu wa nguvu hakuna kingine zaidi ya urafiki wa kawaida, manenomaneno ni kawaida kwa wanadamu,” alisema Lulu.

Batuli Afunguka Kuhusu Tetesi ya Yeye Kuvunja Uchumba wa Rose Ndauka


Stori: RHODA JOSIAH
MSANII wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ameshangazwa na madai kuwa, anahusika kuvunjika kwa uchumba wa msanii mwenzake Rose Ndauka na kueleza kuwa hayo ni maneno ya watu wasiomtakia mema.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni kufuatia madai hayo, Batuli alisema hajawahi kuwa na uhusiano wowote na bwana wa Rose (Malick) na kwamba ukaribu wao ni wa kikazi tu.

“Jamani siwezi kutoka na mchumba wa Rose kutokana na kwamba ni mtu ambaye namheshimu sana na tumekuwa tukifanya kazi na Rose bila matatizo yoyote. Hizi taarifa zinanishangaza na najua wanaozieneza hawanitakii mema,” alisema Batuli.

Didas Fashion Amshukia Clouds 112 wa Bongo Movies , Asema Amelamba Ndimu na Kufunguka Mazito


Kupitia ukurasa wa Didasfacion wa Instagram Jana , Mwanadada huyu aishie UK ..Amefunguka Makubwa Kuhusu Bongo Movies hususan Muingizaji Clouds 112...Jisomee Mwenyewe Hapo chini:

"Hahahaha @eshasbuheti na wewe umejitoa kwa ajili yangu kama @stevenyerere2 au?. Mungu huyu analipa hapa duniani. ... Nina mengi ya kuongea alafu mie huwa siongei kwa maneno naongea na evidence. Nina dhambi za mtu natembea nazo na siku kichaa kikinipanda nitazimwaga hadharani, watu wataacha midomo wazi. Watu wanavaa majoho ya mungu kujifanya wema. Na hapo ndio mtajua kwanini movie yangu ya Mateso Yangu Ughaibuni sijaitoa mpaka leo. Nilinyamaza, ila subirini ma evidence yanakuja. Mi mstaarabu ila ni Kiazi kibovu mnooo.

Nasema nimeramba ndimu, nimechoka sasa ni wakati wa kutapika, naomba waandishi wa habari msogee huku kwa page yangu haraka. Maana ule muda muwafaka umekaribia. Mimi ni Mmanyema halisi. Nimekaa kimya nimechoka. Hawa ni wanawake wenzangu. Pole sana @sabrinarupia alafu ninavyo kupenda wewe dada acha tu. It's time.

Jamani mnamuona huyu kaka hapa? Huyu kaka anaitwa Frank kwa wale msio mjua. Huyu kaka ndio alikuwa aje UK kucheza movie ya MATESO YANGU UGHAIBUNI. Na tulisha kubaliana hadi bei maskini na kila kitu kilikuwa poa. Mara ghafla nikapokea simu ya kinafki, na wakati huo mie nilikuwa sijui lolote kuhusu bongo movie. Nikaambiwa huyu kaka ninae taka kumchukua hajui kucheza wala ku direct movie. Nika pampiwa vibaya mnoo mpaka nikatia akili. Frank kokote ulipo naomba unisamehe najua ulikuwa tayari umekuwa na tamaa ya safari ya kuja ulaya, ila waziba rizki wakafanya yao. Wacha naishi hapo. Hii ni intro tu. Hadithi kamili inakuja. Kaeni na ndimu zenu.
-----------------------------------
Clouds 112 Haya uliniita mimi tapeli tena mzulumati, nimekudhulumu million 8 za kuja kucheza movie, ukaenda mpaka kwenye magazeti kusema, nikapigiwa na wenye magazeti, nikawapa ukweli na ushahidi. Tena huu ni mfano tu, ninazo nyingi na za aibu, na bado naendelea. Frank aliniomba nimlipe Tsh 2 million kucheza hiyo movie, nikakubali, wewe ukasema kila kitu utafanya bure ila nikisha uza movie nikufikirie, sasa leo umemfanya @stevenyerere2 kajiuzulu eti kisa kanisaidia uzinduzi, na hela ya PSPF tumekula, huu ni mfano nakuja kumwaga mengi. Ulijitole kila kitu bure uje ulaya, leo umenipaka mavi dunia nzima mimi tapeli, unawafanyia fitna watu wote wanao kaa karibu na mimi. Hii ni haki? Sawa mimi tapeli dhulumati, zote ni njia za kutafuta riziki. Tutafika hata mahakamani. Bado na rudi na mazito zaidi. Ongezeni ndimu


Clouds 112 Nilihangaika kwa nguvu zangu ili nifanye kitu tofauti. Nahangaika na familia yangu. Hata kama movie niliicheza kimaskini, kwani nyie movie zenu mnazicheza kitajiri? Nimeiba, nimenyang'anya, nimekopa kukupandisheni ndege kuja kucheza movie. Kuna matajiri wangapi wana hela zao na visa kupata hawapati? Wangapi wanaingia ubalozini wanakosa visa. Eti unaaenda kumwambia distributors wasichukue movie yangu kisa umedhulumiwa. Unaweza wewe kuzilipa gharama zangu hata kama ni ndogo? Rizki yangu ninavyo itafuta unaijua? Ninavyo hangaika kutafuta maisha na kupigana usiku na mchana unajua? Hujaziba bado rizki yangu ya hiyo movie, mungu akiniandikia hata Kenya watanunua na wata distribute, karoge sasa. Am sick and tired. Nime nyamaza ila nimeshindwa kuvumilia. Wapenzi wangu naomba mnisamehe. Nahangaika kutafuta riziki nile kwa jasho langu na nguvu yangu. Sijakutuma unipe offer yakucheza movie bure ili ukalalamike. Sijamaliza evidence. Mpaka za mapenzi pia. Nakuja nazo

Nadhani Kuna haja ya Kusikia Kutoka Upande wa Pili wa Clouds 112...

Steve Nyerere: “Bongo movie watanikumbuka


MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa ana mengi ya kujivunia katika klabu hiyo ambayo anaamini yatawafanya wasanii wakumbuke kipindi cha uongozi wake.

Akipiga stori na paparazi wetu, Steve alisema kuna vitu vingi ambavyo ameifanyia Klabu ya Bongo Movie ikiwemo kurudisha heshima katika jamii kwa ujumla kuwa klabu hiyo haihusiani na vitendo vya kifuska bali ni wasanii wanaojiheshimu na kuthamini kazi zao kwa kukemea maovu.

“Naamini wasanii wa Bongo Movie watanikumbuka kwa mengi niliyowafanyia, hata kama wanatazama mabaya yangu lakini yapo na mazuri ambayo ni wazi hayapingiki, niliondoa matabaka pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ni wazi jinsi ilivyo sasa ni tofauti na nilivyoingia madarakani, nimewakutanisha na fursa mbalimbali na kusimamia nidhamu,” alisema Steve.

Hivi Ndivyo AUNTY EZECKIEL alivyotokelezea katika happy birthday ya Wema - Ni Shida.

IMAGE CREDITS:BESTIZZO

Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options

BMW LA WEMA UTATA MTUPU

Achana na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya ‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa ndani ya Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa na meneja wake.
NYUMBANI KWA MADAM
Pati hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Katika shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina, walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.
NISSAN MURANO
Akiwa Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.
Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo Mumy...tafadhali pokea hicho kidogo hiki nilichojaliwa leo.”
BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.
Martin Kadinda akionyesha funguo ya Gari aina ya BMW aliyomzawadia Wema.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni mingi.
Baada ya kuona hivyo, Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.
MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.
Muonekano wa keki ya ‘bethidei’ ya Wema.
Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata, kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram akaandika:
“....Gari hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao....”
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akimlisha keki mama yake.
MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”
MASWALI
Huku Kadinda akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa mastaa walioalikwa (jina kapuni).
Akimlisha keki mamamkwe wake.
MENGINE YATOKANAYO
Pati hiyo ya Wema iligawanyika mara mbili ambapo ya kwanza ilianza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 huku nyingine iliyohusisha watu maarufu ikianza baadaye hadi ‘kokoriko’.
KEKI 69 MEZANI
Katika hali isiyo ya kawaida, sherehe hiyo ilikuwa na keki zipatazo 69 ambazo zililetwa na baadhi ya mastaa ambao walihudhuria sherehe hiyo huku kukiwa na vinywaji vya kufa mtu (wiski tu), loko bia tupa kule.
Akimlisha keki Jokate.
NDAFU
Kwa upande wa nyama kulikuwa ndafu mzima ambaye watu walimtafuta hadi wakasaza.

MAMA DIAMOND AMTANGAZA RASMI MKWEWE  
Katika sherehe hiyo, mama Diamond alipopewa kipaza sauti ‘maiki’ ili anene chochote alisema kuwa Wema ni mkwe wake wa halali na kwamba anampenda hivyo asiwe na wasiwasi kwani hakuna mkwe mwingine atayatokea zaidi yake.
Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akifungua shampeni kwaajili ya shughuli hiyo.
“Jamani huyu ndiye mkwe wangu, Mrs Chibu (Diamond) ndiye mkwe wangu hasaaa...,” alisema mama Chibu huku watu wakishangilia.
MILIONI 10
Kwa mujibu wa Kadinda, shughuli hiyo iligharimu zaidi ya Sh. milioni 10 hadi kukamilika na kuonekana ya tofauti na pati nyingine za mastaa Bongo.
Wema akiongea jambo kabla ya kukata Ndafu.
AMWAGIWA NOTI
Ulipofika muda wa kutunzwa zawadi, watu walijitokeza kumtunza Wema fedha ambazo hazikuweza kupatikana kiasi chake mara moja huku staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiweka rekodi kwa kumwaga ‘minoti’ mingi katika hafla hiyo.

Video: Irene Uwoya na Mwigizaji Rich Wapigana Denda Live Live

Kama mpenzi wako ana ndoto za kuwa muigizaji wa filamu za hapa Tanzania, huenda ukabadilisha mawazo yako ukiona video hii ya Irene Uwoya na Single Mtambalike aka Rich wakibadilishana mate kwenye scene ya filamu yao mpya.

Wema Sepetu 'Watu Wenye Majungu Hawanisumbui Kichwa Kabisa Nabaki Nawatazama Tu'


Stori: Mayasa Mariwata
MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi.

Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.

“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.

SIKILIZA NA DOWNLOAD: New AUDIO | Wimbo Wa LULU[Elizabeth Michael].

TAZAMA PICHA ZOTE ZA BIRTHDAY PARTY YA WEMA SEPETU...



Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options




Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options

ZAWADI YA GARI>>>>>HAPA

‘I Should Have Known’ – Wema Sepetu Apost Ujumbe Uliowafumba Wengi Instagram


Kuna tetesi kuwa Wema Sepetu na Diamond Platnumz hawapo tena pamoja. Magazeti ya udaku yameandika kuwa Diamond anataka kuoa.. lakini mwanamke anayetaka kumuoa si Wema, ni Meninah! Hatujaweza kuthibitisha ukweli wa tetesi hizo lakini kuna dalili nyingi kuwa hakuna amani tena paradiso.

Tetesi za kuvunjika kwa power couple hiyo ya Bongo, zimechochewa zaidi na post ya mafumbo ya Wema Sepetu kwenye Instagram. Katika post hiyo, Wema ameweka picha yenye rangi nyekundu pekee yake na kuandika ‘I shouldve known’.

Picha hiyo imezua maswali mengi kwa followers wake zaidi ya 211,133 kwenye mtandao huo unaopendwa Tanzania.



Haya ni baadhi ya maoni:

modestae68

@wemasepetu haya mbwa mwitu huyoooo katoka hakuna cha princess sasha,superstar wala ile filam uliyosema unacheza kama mgonjwa wa kansa ukanyoa kipara yaani naumia kuona hivyo wema vp? Acha mambo ya kugawa pesa majukwaani sio wote wanaokushangilia unapopanda ktk majukwaa wengine wanakuzomea hukui? Acha kulewa sifa za team za kukusifia kila ufanyalo yaani sijui niseme nn nikiona wenzio wanavyosonga mbele naumia alafu wewe unaonyesha ufahari majukwaani mmmh kweli hakuna kizuri kinachokosa kasoro haya watakaonitukana poa tu lkn mm wema ni kama mdogo wangu nampenda sana ndio maana namwambia sasa wale waliozoea kutukana tukaneni mpaka mchoke lkn nyie nyie mlikuwa mnasema ktk kampen ya bring our wema hivyo sitoshangaa.mm nitaongea mpaka siku nikiona mabadiliko nafikiri ndio siku nitakayoridhika japo ni kwa faida yake na siyo yangu ila sio mbaya kumwambia mtu kitu chenye faida kwake hata kama huna faida nacho.am still love u wema.

mwelumwikya

I saw this coming @wemasepetu you are a beautiful girl with brains you should not worry at all he is only 25

patrarobert

sitaki kuamini kuwa uko kwenye majuto…na hasa kama majuto yenyewe yanahusiana na mahusiano yako ya kimapenzi….bt kama ndivyo;kwanza pole…kila kitu knatokea kwasababu…angalia ulipojkwaa,nyanyuka futa vumbi…anza upya…Kama n jambo lingine…do the same:ILA U BETTER START LIVING…START ACTING LIKE A LADY…kila mtu ana kasoro zake…n kweli ila zako znaonekana zaidi kwa sababu u r on spotlight…na kwasababu u r an attention seeker…achana na hayo mambo wema…sitaki kuamini kuwa wewe n sikio la kufa…tuko wengi yametukuta mengi sababu ya kutosikiliza wazazi…kusema tu “nampenda mama angu,she z my everything”bila kumtii na kufuata maagizo yake n bure…na AMINI kuwa u wont rest mpaka ukianza kumtii mzazi wako…kama ni huyo diamond atakusumbua mpaka uchanganyikiwe kwasababu huo uhusiano hauna baraka za mama ako…unaweza ona kama kakuruhusu…inabidi akuache ufanye utakalo ili dunia ikufundishe…HUJACHELEWA… @wemasepetu @wemasepetu

callyrissanen

Sijui unachokiongelea kama ni majuto au surprise nzuri. Cha muhimu nakwambia kama dada mkubwa lol, acha starehe za kugawa pesa kwenye kadamnasi. Wekeza hizo pesa uende vacation hata hapo PARIS TUU wewe na umpendaye, sio lazima awe baby yako chibu. Weka pesa na ujijengee tabia ya kutoka outings za kwenda kwenye hotel nzuri kula chakula kizuri wewe na familia yako au mtu umpendaye, sio lazima awe baby yako Chibu. Weka pesa nenda gym kujikeep busy angalau mara 3 kwa wiki, sio lazima na baby yako chibu kwani utapata personal trainer. Weka pesa na acha kuwanufaisha hao wacheza show kwani ukifulia watapata maneno ya kutungia wimbo. Take care and remember that;this too shall pass!!

magz_16

You all need to leave these two have fun and enjoy each other as it lasts.Diamond is still a young boy…!!!How old is he again!!!Hes got a looong way to go as a man.@wemasepetu ….if i were you..i would just focus more on making money and building my future!!Build a house…be a business woman…date real men that will not be intimidated to help me rise up there….I would make money more than even Diamond himself…I would rise like i have never before..and why?coz i carry a powerful name…iam beautiful..and Educated too.I wouldnt go clubbing splashing money on artists..i will go out there make money than all my exes…and my current boyfriend.I would make sure…east Africa knows who # Wema..as a Brand..and not just as diamond girlfriend.I wish you all the best sweetie….stay Focus

Unahisi anajuta kurudiana na Diamond na huenda wakawa wameachana kweli? Tupia maoni yako.

Kajala: Watu Wanaamini Sana Magazeti, Sina Utajiri Huo Wanaousema na Siwezi Kumwajiri Wema Sepetu

Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.

Muigizaji huyo wa filamu alisema kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri Wema Sepetu ni uzushi mtupu. “Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,” Kajala aliiambia Bongo5.

“Mimi naona nipo vilevile hakuna kubwa sana lililongezeka. Nafanya shughuli zangu tu. Tatizo watu wanaamini sana magazeti. Mimi i sina utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala ni yule yule,” alisisitiza.

Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.

KIVAZI HIKI CHA JOKATE CHAZUA GUMZO MTAANI!

MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata baada ya kupiga picha akiwa ametinga suruali iliyochanika.
Mwanamitindo na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo.
Akizungumzia picha hiyo ambayo imevuja katika baadhi ya mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi karibuni Afrika Kusini alipokuwa amekwenda kurekodi wimbo wake mpya (hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili kuonesha utofauti.
Jokate Mwegelo akipozi na mzungu.
“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata watu wengi walikuwa wakijiuliza kulikoni mimi kuvaa hivyo  lakini mimi nafikiri lazima kuna wakati tunatakiwa kuonekana tofauti na siyo mapambo muda wote ukibadilika hata unachofanya unakuwa tofauti,” alisema Jokate

MAMA KANUMBA AFICHUA MAZITO YA RAY, MWANAYE

BAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:
“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla  hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.”

MSIBA WAZIMA MBWEMBWE ZA AUNT MAREKANI

Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake aliyefariki dunia juzikati.
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa mamtoni.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za mdogo wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye mazishi.
Ijumaa lilipata bahati ya kuwasiliana na Aunt ambaye alisema ameshitushwa na taarifa hizo na alikuwa njiani kurejea Dar.“Nimeumia sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu tuliyependana sana lakini Mungu kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa masikitiko.

Wema Sepetu:Wanaoniponda Wengi Wao Wanatumia Tecno na Huawei


Katika hali iliyoshangaza wengi,beautiful oninye mwenye endless fame mnyange Wema Sepetu amesema watu wengi wanaomsema kwenye mtandao they don't have life na wengi wao wanatumia Tecno na Huawei kulog in kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumponda, akichezesha taya na Ephraim Kibonde katika kipindi cha jahazi amesema watu hao hawampi shida hata kidogo kwani wamepigika na yupo juu zaidi yao.

My Take:Hivi Sister wema hizo simu ulizozidharau unazijua vizuri kweli? Hivi unaweza ku-compare features za Huawei Ascend P7/Tecno H7 na Samsung Gallaxy S4?

BAADA YA NORA KUWABEZA BAADHI YA WASANII, YUSUPH MLELA AIBUKA NA KUMPIGA DONGO NORA NA KUMUITA "KIBIBI"


KUFUATIA madai ya hivi karibuni ya mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuwa baadhi ya waigizaji hawana sifa za kuwa wacheza sinema zaidi ya kuuza sura, msanii Yusuph Mlela amempa dongo zito akisema licha ya umri kuwa mkubwa, pia ana matatizo flani yanayomsumbua.

“Nora naona siyo kosa lake kwani alishaugua yule,  isitoshe ameshakuwa bibi hivyo nimemsamehe na sina tatizo naye kwani najua, lingekuwa jambo la maana kama angetufuata na kutushauri kama mkongwe lakini si kwa njia aliyofanya,” alisema Mlela.

Hivi karibuni Nora aliwataja mastaa wenzake wa filamu akiwemo Mlela, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Kajala na Batuli akisema hawawezi kazi zaidi ya kuuza sura tu.

JOKATE MWEGELO,IRENE UWOYA,ADAM KUAMBIANA NA JB WAKUTANA KWENYE FILAMU YA MIKONO SALAMA, JIONEE HAPA


Tarehe 25.09.2014 Filamu kali na yenye kusisimua "MIKONO SALAMA" Itaingia kwenye Soko la Filamu za kitanzania na kuanza kuuzwa.Sio Filamu ya kukosa kabisa kwani Humo ndani kuna waigizaji mashuhuri na Magwiji ambao wameshirikia na Mastar kutoka pande zingine.Jokate Mwegelo maarufu kama Kidoti ameshiriki ndani ya Filamu hii akiwa na 


Gwiji Jacob Steven(JB),pia kuna kipande ambacho amecheza Marehemu Adamu Kuambiana humu ndani,pia Kuna wasanii wengine kama Irene Uwoya na Single Ntambalike.Kaa Tayari kuona Filamu nzuri na yakitanzania.

JACKLINE WOLPER : I Feel so Good to Chat With Him When Am Like This..


  Bongostarslink imeakutana na Picha hii ya JACKLINE WOLPER kwenye account ya instagram kwa jina wolperstylish yenye Caption: I feel so good to chat with him when am like this..

"KUJIUZULU KWA STEVE NTERERE NI PIGO KWA BONGO MOVIE , HAKIKA TUTAYUMBA"..MSANII CATHY AFUNGUKA

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.

“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.
GPL
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX