Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label bongofleva. Show all posts
Showing posts with label bongofleva. Show all posts

Ben Pol adai uhusiano wa miezi 9 na Latifa ni mrefu zaidi aliowahi kuwa nao tangu awe staa


Uhusiano na mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2013, Latifa Mohamed wenye miezi tisa sasa, ndio uhusiano mrefu zaidi aliowahi kuwa nao Ben Pol tangu awe staa.

Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa mahusiano yake yaliyopita yalishindwa kudumu kwakuwa wasichana wengi walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwake kwakuwa yeye ni msanii. “Sasa hivi tuna miezi tisa, nadhani ndio the longest relationship,” amesema Ben kuhusu uhusiano na Latifa.

“Unajua nimekutana na watu wa aina tofauti. Nimekutana na watu ambao labda wanakuwa na expectations kubwa zaidi kuhusu mtu fulani, kwahiyo akiingia kwenye maisha yako labda kuna vitu ambavyo yeye tayari alishapicture, ‘labda Ben Pol tutakuwa tunakula bata every weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku kule everyday. Kwahiyo mtu anaweza akaja kwenye maisha yako akakuta sio mtu wa hivyo, ni staa ndio lakini you don’t go to clubs mara kwa mara, you don’t do this, you don’t do that kama mastaa wengine. Kwahiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye maisha yako. Ndio hicho ambacho nimeexperience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita.”

“Kwahiyo ukipata mtu ambaye akakuelewa hivyo, inatia moyo kidogo.”

Ben Pol amesema hata hivyo uhusiano wake na Latifa haujawa rasmi kabisa kwakuwa bado hajaenda kujitambulisha kwao.

“Lakini at least naweza kusema nina hatua moja katika tano au katika tatu.”
-Bongo5

DIAMOND AFANYA MAKAMUZI YA NGUVU BIG BROTHER HOTSHOTS



Diamond Platnumz akifanya makamuzi ndani ya Big Brother Hotshots.
STAA wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku huu amefanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi wa shindano la Big Brother Hotshots unaofanyika jijini Johanessburg nchini Afrika Kusini.
Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na watu wawili mrembo Irene 'La Veda' na Idriss. Jumla ya washiriki 26 kutoka mataifa 12 ya Afrika watachuana kwa siku 63 kutafuta mshindi atakayejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 300,000.

BIRTHDAY YA DIAMOND, BEATIFUL ONYINYE WEMA SEPETU AZUA GUMZO!..TAZAMA PICHA NA VIDEO YA KILICHOTOKEA

Stori: Waandishi Wetu
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’.
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Diamond Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya pamoja.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake.
Saa 3:30 USIKU
BUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei.
SAA 4:00 USIKU
BIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh! Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani.
SAA 5:00 USIKU
SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
Nuh Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo.
Risasi Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKU
NGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Wageni waalikwa wakizidi kuingia ukumbini.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki ya Bethidei ya Diamond.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.

Hii Ndio Zawadi Aliyopewa Diamond Kwenye Birthday Yake, Kwa Taarifa yako Haikutoka Kwa Wema


Jana Ilikuwa Ni Siku ya Kuzaliwa ya Mwanamuziki Anaye Make Headlines Bongo na Nje ya Nchi Diamond Platnumz, Hakika wengi Walisubiri Kuona Mpenzi wake Wema Sepetu Atamzawadia Zawadi gani Kwa Vile Yeye Alizawadiwa gari na Diamond..So Wengi Tulisubiri kuona Atafanya nini ....Lakini Jana Zawadi kubwa iliyotolewa ilikuwa ni Gari Aina la BMW ambalo Diamond Alipewa Zawadi na Management Team yake ..Ikimaanisha kina Babu Tale....Mie Sikuwepo kwenye Party Hiyo kwa anayejua Wema Alitoa zawadi Gani Atujuze Basi Hapo Kwenye Comment.

Kiingereza cha Diamond,The Sporah Show na Kile Cha Shigongo, Straight Talk Africa

Well,inatia moyo kuona waswahili sasa tunaanza kuwa majasiri wa kufanya interview za kiingereza(JAPO BROKEN) na hasa ujasiri huo unapofikia hatua ya kufanya interview katika vipindi vya TV vinavoangaliwa na watu wengi duniani kote.So,jana tar.30/9 nilimsikiliza Diamond akiamua kuwa jasiri na kupima uwezo wake wa kukimudu kimombo pale alipofanya interview ya kimombo na Mrembo Sporah Njau wa The Sporah Show kinachorushwa Clouds TV kutokea London.

Na wakati huu namsikiliza Eric Shigongo akifanya interview na presenter mahiri wa kipindi cha Straight Talk Africa,Prof Chaka Ssali wa The Voice of Africa.Nawapongeza kabisaaaaaa but man,we can still pick a hole or two in the interviews: (1).The guys are trying too hard to impress and to sound relevant,nafikiri wakati mwingine wasipanie au wasiwe na fikra kuwa ndugu zao tunaowaangalia huku tuwakome,i mean wafanye interview wakiwa totally focused on the issues raised in the interviews na wasitake tunaowasikiliza "tuwakome" (2).Sporah alizungumza Queen's English wakati Diamond alitaka watazamaji tuamini kuwa yeye ni Kanye West au 50 Cent.

Hivyo hivyo Eric Shigongo wants us to believe kuwa yeye ni wa mitaa ya Brooklyn New York wakati yeye ni Msukuma through and through....ninachosema,they need not fake their accent,mbona Chaka Ssali ni profesa na anazeekea Marekani lakini hathubutu kusema accent ya kimarekani?

Yeye bado anapiga kiingereza chake cha Kabale Uganda and he's doing good!Nasema hivi,wanastahili pongezi lakini wazungumze kiingereza cha kawaida tu wasitake kutafuna maneno kama kina Obama,kufanya hivyo kunawaboa viewers because for one,they are not fluent,sasa kama hauko fluent utatakaje kujiongelesha accent ya kimarekani,people!Wanigeria na Wakenya mbona wanaongea tu kivyao vyao and we have come to like Nigerian English'oooo,haven't we?

Hongera Diamond,hongera Shigongo,mna afadhali kuliko Mh.Membe,siku moja nilimsikiliza kwenye kipindi kilekile cha Straight Talk Africa niliboreka sana,sikuona tofauti yake na Mulugo

Dada wa Diamond Esma Atoa Mipasho Kupitia Instagram Wiki Mbili tu Baada ya Kuolewa

Dada wa Mwanamuziki Diamond Anayejiita Esma Plainum Ambae Ameolewa Hivi Karibuni na Petit Man Amepost Video Kwenye Instagram Page yake Huku Akitoa Mipasho ya Taarabu yenye Kuwananga Wanao Ona Wivu Juu Yake Kuolewa...Baadhi ya Maneno yanasikika Akiimba
'Mwaona Donge la Nini Kama Mnaweza Pandani Juu mkazibe'

Je Kunani Tena ? 

Jionee Mwenyewe Hapa:
((bofya hapa))

HIZI NDIZO PICHA ZA AWALI ZA KILICHOJIRI KWENYE BIRTHDAY YA DIAMOND - ZIANGALIE HAPA









DIAMOND ACHARUKA BMW LA WEMA!

Ni sheeedah! Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amecharukia gari aina ya BMW 545 alilozawadiwa mwandani wake, Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, akipinga gari hilo kupewa na meneja wake, Martin Kadinda.
Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake, Martin Kadinda.
DIAMOND ACHANGANYIKIWA
Habari za kipekepeke zilidai kuwa, taarifa ya Kadinda kumpa zawadi ya gari Wema kwenye pati ya bethidei yake Jumapili iliyopita, nyumbani kwake, Kijitonyama, Dar zilimchanganya Diamond na kudai kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani kwa maana anamfahamu vyema Kadinda kuwa hana uwezo huo wa kununua BMW la zaidi Sh. milioni 56 za madafu.
Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akifungua shampeni katika bethidei yake.
Chanzo hicho kiliweka wazi kwamba mkali huyo anayekimbiza na Ngoma ya Mdogomdogo alihamaki baada ya kupata taarifa kuwa siyo yeye peke yake aliyekabidhi zawadi ya gari (Nissan Murano) kwa maana aliamini mwenye zawadi ya gari alikuwa ni yeye tu ambayo ilikuwa ‘surprise’ kwa mpenzi wake huyo.
Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’akipokea funguo ya gari la zawadi kutoka kwa Meneja wake.
BOFYA HAPA KUPATA ‘UBUYU’
 “Unaambiwa Diamond kachanganyikiwa kabisa kusikia Wema kapewa gari, tena BMW na mbaya zaidi aliyempa gari ni Kadinda huku yeye akiamini kabisa zawadi aliyotoa kwa mpenzi wake asingeweza kupata kwa mtu mwingine yeyote, mwenyewe anasema amedhalilishwa kwani hawezi kutoa gari kisha mwanaume mwenzake naye atoe gari,” kilidai chanzo hicho.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
Mpashaji huyo alizidi kufafanua kwamba baada ya kupokea taarifa hizo na kuona kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali akiwa nje ya nchi, Diamond alianza kufanya utaratibu wa kurudi nchini akitokea Canada ili kujua vizuri kuhusu undani wa hilo gari.
“Yaani ninyi mtasikia, nakwambia kimenuka maana Diamond aliposikia na kusoma habari za BMW la Wema alianza kufanya utaratibu wa kurudi Bongo ili kupata ufafanuzi zaidi,” kilisema chanzo hicho.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
KADINDA AKOMAA
Kwa upande wake Kadinda ameendelea kusisitiza kwamba yeye ndiye aliyenunua gari hilo na kumkabidhi Wema ikiwa ni michango ya watu wanaomsapoti mwanadada huyo.
Kuhusu gari hilo, watu kibao wamekuwa wakitajwa kulinunua akiwemo mfanyabiashara Mkongo mwenye jina linaloanza na herufi S na mume wa mtu ambaye ni kigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar anayetajwa kwa herufi moja ya L.
WEMA VIPI?
Jitihada za kumsikia Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo hivyo juhudi za kupata lake la moyoni zinaendelea. Stay tuned kwani inavyoonekana nyuma ya pazia ya gari hilo kuna siri kubwa!

Happy Birthday Diamond: Mmanyema mwenye uchaga kipesa, uhaya kisifa na uzungu kikazi - Msikilize Pia diamond Akifunguka Hapa.

Kwa mujibu wa meneja wake Babu Tale, Diamond ni mmanyema mwenye uchaga kipesa, uhaya kisifa na uzungu kikazi.
“Acha niseme hili tangu siku tunakutana mpaka leo aujawai kukosa kunipa shikamoo ni ishara ya heshima ya kweli na sio ya kuigiza,” ameandika Tale kwenye ujumbe wa kumpongeza staa huyo kwenye siku yake ya kuzaliwa, Oct 2.
Staa huyo anafanya bonge la party kujipongeza leo na pia ametoa nafasi chache kwa mashabiki wake kuhudhuria.
“Najua wote tungependa tufurahie kwa pamoja siku yangu hii ya kuzaliwa, lakini kwa bahati mbaya hakuna ukumbi utaoweza kututosheleza… sasa tafadhali naomba niambie, unahisi ni kwanini nikupatie wewe kadi hii ili uwe muwakilishi wa Mashabiki zangu??? (nataka nitoe kadi kwa watu 5),” ameandika kwenye ukurasa wa Facebook.
Diamond anasherehekea siku yake ya kuzaliwa siku chache tu baada ya ile ya mpenzi wake Wema ambapo alimzawadia gari jipya. Kupitia Instagram, Wema ameandika: Happy Birthday to you my original soul… ngoja nitulie kwanza ndo niandike caption maana nina mengi kwa kweli… ila jua nakupenda sana…
((BONYEZA HAPA KUMSIKILIZA)) 

Hii Ndio Sababu ya Clouds FM kushindwa Kumtumia Diamond Kwenye Show zao za Fiesta


Wakati wasanii wakibongo kwa ujumla wao wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu, Diamond ameendelea kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi cha jamaa wa Clouds Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu kwenye show zao!

Ieleweke kwamba kipindi hiki huwa ni cha neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine hufikia kuomba angalau tu wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani kuonana na mashabiki.

Diamond kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje ya nchi kiasi kwamba imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki show za hapa. 

Pamoja na upizani mkubwa mno naoupata kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata kwa wale ambao bado walikuwa wabishi kumkubali Diamond.

Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumtakia mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi makubwa kabisa kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.

Haya Ndio Majibu ya Wema Sepetu kwa wale wote Wanaomshambulia Mtandaoni kuhusu kupewa BMW " Mnapotangaza Vita __"



Zawadi ya Gari Aliyopewa Wema Sepetu Siku ya Kuzaliwa Yaleta Kizazaa, Wadada Wamjini Wamecharuka


Juzi ilikuwa ni Siku ya Kuzaliwa kwa Mrembo Wema Sepetu, Kitu kilichovuta Hisia za Watu wengi ni zawadi ya Gari aliyopewa Wema Sepetu kutoka kwa Mpenzi wake Diamond Platnumz...Inasemekana huko mjini wadada wamechachamaa hawataki tena zawadi mchwara za maua , visimu ama saaa siku za sikukuu zao za kuzaliwa nao wanataka magari nao kutoka kwa Maboifriend zao.

Hili ni Tamko la Umoja huo wa Magelofurendi :

Pic of The Day: Mwanamuziki Recho Katika Pozi Ofisini


Mwanamuziki Recho Katika Pozi Ofisini, Haikuweza Kufahamika ni Ofisi gani ila Mazingira yanaonesha ni ofisi fulani...Kivazi hicho Jamani Chanimalizaaa

BAADA YA KUPIGWA MADONGO KUWA ALIKUWA ANADANGANYA WEMA SEPETU AMEONESHA KADI YA GARI ALILONUNULIWA NA DIAMOND PLATNUMZ

Baada ya jana mwanadada wema sepetu kupewa zawaidi ya Gari aina ya NISANI -Murano....ilivumu kuwa iliilikuwa zuga tu..kutokana na kile kinachodaiwa ni kutafuta KIKI...Sasa leo kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM manager wa mwanadada huyu, Martin Kadinda amefunguka baada ya kutupia picha hii ;.
"Yes…. Not only Murano from ya baby @diamondplatnumz this BMW is yours yes…. Suprised kuona jina kwa kadi?? I meant it… this car came from kazi ndogo tufanyazo na support kubwa ya watu who wish you the best always… peke yangu nisingeweza bila support yao. One thing you should know nimejitolea kufanya kazi na wewe
because naamini kwa tanzania ur my number one celebrity and my wish is to see u living as a truly superstar…. Make my dreams come true basi.. Wema mimi natembelea vimeo lakini siwezi kukubali wewe ushuke huku.. Wema its hight time u stand and this is high time to understand kuwa wewe ni star and u deserve the best from ya fame…!! People loves u so much….."

HILI NDILO JUMBA AMBALO DIAMOND AMEMJENGEA MAMA YAKE MZAZI..LICHEKI HAPA JUMBA HILO


kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond ametupia picha ya ile nyumba aliyosema anamjengea mama yake. Katika picha hiyo aliambatanisha na maelezo haya "Had to visit mama Chibu's Village today.." Nyumba hiyo inaonekana ya kifahari hasa ukiangalia muundo na mabati yaliyotumika kujenga nyumba huyo.


RECHO AMRUHUSU SHABIKI KUMFANYA LIVE KWENYE STAGE SASA HIVI NDIVYO JAMII UNAVYOIELIMISHA DADA RECHO?

 
 

BABY MADAHA ATAMANI PENZI LA WEMA, DIAMOND

MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha BongoBaby Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.
Mwanamuziki mwenye vituko kila kukicha Bongo,  Baby Joseph Madaha akipozi.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua ya kuwaonea wivu.
Wema Sepetu na Nasibu Abdul, ‘Diamond’.
“Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.

FIESTA YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA SONGEA


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Recho akifanya makamuzi kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa majimaji, Songea.
Recho akiwajibika yake jukwaani.
Mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Songea.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akiwa amekumbatiwa na shabiki wake.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akicheza na mmoja ya shabiki wake Ole Themba.
Mashabiki wakiendelea kupagawa na burudani.
Msanii wa Bongo Fleva, Mo music akitoa burudani kwa wakazi wa Songea.
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX