Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

WASANII WA FIESTA WATINGA KATIKA OFISI ZA MKUU WA MKOA WA SONGEA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu (katikati) akiongea na wasanii wa Fiesta (hawapo pichani) asubuhi ya leo muda mfupi baada ya kuwaomba kunywa nao chai Ikulu ndogo Songea.
Wasanii wa Serengeti Fiesta wakiendelea kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Mkurugenzi wa utafiti na maendeleo wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba(wa pili kutoka kushoto) akiwaongoza wasanii wa Serengeti Fiesta Ikulu ndogo Songea.

ASKARI WATATU WAJERUHIWA KWA MLIPUKO WA BOMU SONGEA

Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi

Eneo la tukio likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao.
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini

ASKARI watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.

Tukio hilo limetokea September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja laMatarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu waliokuwa doria.

Askari hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu. Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendohicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitiavyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.

FURSAA..!! NAFASI ZA KAZI ZA MITINDO NA UIGIZAJI..SOMA ZAIDI KUJUA JINSI YA KUPATA NAFASI


Wewe ni msichana mwenye kipaji cha mitindo lakini haujui uanzie wapi? Wewe ni msichana mwenye kipaji cha kuigiza ? Unatafuta nafasi ya kuigiza kwenye filamu ? Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako.


Kampuni inayo jihusisha na ku- manage wanamitindo pamoja na wasanii wenye vipaji mbalimbali inatangaza nafasi za kazi zifuatazo :


A. WANAMITINDO WANAWAKE ( FEMALE MODELS )
Sifa za wanamitindo wanao hitajika :
i.Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.


ii.Awe wa jinsia ya kike


iii.Awe anaweza kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na kiingereza.


iv. Awe na passion na kazi ya mitindo.


MAJUKUMU YA KAZI :
Kufanya kazi za mitindo katika projects mbalimbali za kampuni zilizopo ndani na nje ya mkoa wa Dar Es salaam pamoja na nchi jirani.


B. WASANII WA FILAMU.
Sifa za wasanii wanao hitajika :


i.Awe wa jinsia ya kike.


ii.Awe na kipaji cha ukweli cha uigizaji.


iii.Elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.


MAJUKUMU :
Kushiriki katika filamu mbalimbali zinazo tolewa na kampuni mbalimbali za utayarishaji filamu.


JINSI YA KUTUMA MAOMBI YAKO
1. Andika maombi yako kupitia barua pepe yetu ambayo ni : neemarecruitmentagency@gmail.com


Maombi yako yaelekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji, Neema Recruitment Agency.


2. Leta maombi yako moja kwa moja katika ofisi zetu zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU mbele ya CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.


JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU :
Kufika ofisini kwetu panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kisha shuka kituo kinaitwa TAKWIMU ukifika hapo tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia utaona ofisi imeandikwa RAEFO TANZANIA.


Kwa maelezo zaidi piga simu 0784406508.

TANZANIA YAWA MIONGONI MWA NCHI ZINAZOTUMIA VIBAYA INSTAGRAM..SOMA KUJUA UNDANI


Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji picha umeendelea kupata mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi kati ya watumiaji hao wameisababisha kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya mtandao huo duniani kote.

Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasialiano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy katika mahojiano maalum aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times Fm.

“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeongoza kwa watu kulalamika kwamba matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na hii inatokana na pale watu ambao wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu wanavyoweka vitu wanavyoweka, ugomvi, matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa watu huwa wanalalamika.” Amesema Innocent Mungy.

“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka record kwamba watu wengi waliolalamika kwenye mtandao huu kuhusu picha za watumiaji ambao wako Tanzania labda ni 20 wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo idadi inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.

Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya kijamii, wakati wa kujiunga mtumiaji hupewa maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya kutumia mtandao huo ikiwa ni pamoja na makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania huwa hawayafuatilii/huyapuuza.

Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia mitandao hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo.

“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni maendeleo. Matumizi ya mitandao sio mabaya ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya. Ningewataka watanzania ambao wanatumia mawasiliano haya vibaya waache. Tuitumie vizuri. Na wale watu ambao unawaona wewe hawaendani na matumizi ambayo yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako. Wa-Unlike, wa-Unfriend au wa-delete kabisa ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi wanayofanya.”

Usikose kusikiliza kwa undani habari hii katika kipindi cha Mtazamo Wiki Hii cha 100.5 Times Fm, Jumamosi hii kuanzia saa moja kamili asubuhi.
 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX