Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » BAADA YA NORA KUWABEZA BAADHI YA WASANII, YUSUPH MLELA AIBUKA NA KUMPIGA DONGO NORA NA KUMUITA "KIBIBI"

BAADA YA NORA KUWABEZA BAADHI YA WASANII, YUSUPH MLELA AIBUKA NA KUMPIGA DONGO NORA NA KUMUITA "KIBIBI"


KUFUATIA madai ya hivi karibuni ya mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuwa baadhi ya waigizaji hawana sifa za kuwa wacheza sinema zaidi ya kuuza sura, msanii Yusuph Mlela amempa dongo zito akisema licha ya umri kuwa mkubwa, pia ana matatizo flani yanayomsumbua.

“Nora naona siyo kosa lake kwani alishaugua yule,  isitoshe ameshakuwa bibi hivyo nimemsamehe na sina tatizo naye kwani najua, lingekuwa jambo la maana kama angetufuata na kutushauri kama mkongwe lakini si kwa njia aliyofanya,” alisema Mlela.

Hivi karibuni Nora aliwataja mastaa wenzake wa filamu akiwemo Mlela, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Kajala na Batuli akisema hawawezi kazi zaidi ya kuuza sura tu.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX