Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Beyonce Ajibu kwa Vitendo Tuhuma za Kuhariri Picha Inayoonesha Sehemu ya Mwili Wake

Beyonce Ajibu kwa Vitendo Tuhuma za Kuhariri Picha Inayoonesha Sehemu ya Mwili Wake

Jana mashabiki walimshambulia Beyonce kwa picha aliyopost kwenye Tumblr ikiwa ni moja kati ya picha za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alizopiga mapema mwezi huu, ikimuonesha akishuka ngazi akiwa ndani ya vazi la ufukweni.

Madai ya mashabiki hao yaliyowekwa kwenye mtandao wa TMZ pamoja na picha ni kwamba Beyonce alihariri sehemu iliyoonesha nafasi kati ya mapaja yake ili aonekane mwembamba zaidi.

“Questionable thigh gap there, Bey. #photoshop #wonkystep #beyonce,”aliuliza shabiki mmoja.

Bado swali linabaki kuwa, je, watu maarufu huamini wanakuwa na mvuto zaidi wanapokuwa wembamba kuliko walivyo na bantu figure?

Masaa machache baada ya tuhuma hizo kuenea, Beyonce aliamua kujibu kwa vitendo kwa picha zinazoonesha uhalisia wa mwili wake na kwamba hakuna ‘Photoshop’.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki kumtuhumu Beyonce na Jay Z kufanya photoshop ya picha zao ili aonekane mwenye mvuto zaidi.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX