Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Diamond Ataka Wema Amzalie Mtoto .....Wema Akataa Kuogopa Kupoteza Mvuto Na Umaarufu, Diamond Amrushia Dongo

Diamond Ataka Wema Amzalie Mtoto .....Wema Akataa Kuogopa Kupoteza Mvuto Na Umaarufu, Diamond Amrushia Dongo





Diamond Platnumz kwa muda sasa amekuwa akimwambia mpenzi wake Wema Sepetu abebe mimba kwasababu yeye anataka mtoto lakini Wema amekuwa mgumu kukubali kudungwa mimba na Diamond kwasasa kwa madai kuwa hayupo tayari kuzaa muda huu sababu ikiwa ni kuwa atapoteza mvuto wake kiumbo na pia kuchuja kiumaarufu, kitu ambacho hakitaki.


Chanzo kilicho karibu na Wema na Diamond kimesema kuwa:


"Ni muda sasa Diamond anataka mtoto tatizo Wema hataki, anaogopa kushuka umaarufu na pia kupoteza umbo lake lenye mvuto.


"Kitendo hicho kimemuweka njia panda Diamond kwa sababu pesa anayo ya kutosha kulea mtoto ila haelewi kwanini Wema hataki wapate mtoto eti kwa kisingizio cha kupoteza fame yake na umbo"

Hata hivyo Diamond juzi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliweka post inayoshabihiana na maelezo ya chanzo hicho. Diamond ni kama alikuwa amerusha Dongo hilo kwa Wema kwa kuandika ...


"Kwa mtazamo wangu mimi naona kuzaa hakumfanyi mtu azeeke au awe wa kizamani, ni tabia tu ya mtu mwenyewe.... na ndio maana dada zetu kama Beyonce, Nancy sumary, Kim Kardashian na kadhalika wana watoto na still wanafanya vizuri.....Au we mtazamo wako ukoje?........ "


Vile vile mapema wiki hii gazeti moja la burudani liliandaka habari inayokaribiana maana na hii kuwa Wema hataki kuzaa kuogopa kupoteza mvuto wake na umaarufu

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX