Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Hatimaye Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Mahusiano ya Kimapenzi na Mwanamuziki Jux

Hatimaye Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Mahusiano ya Kimapenzi na Mwanamuziki Jux

Vanessa Mdee aka Vee Money amekanusha tetesi zilizopo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Nitasubiri’ Jux.

Siku za hivi karibuni, Vanessa na Jux wamekuwa karibu kiasi cha watu kuhisi kuwa ni wapenzi.

“Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu,” amesema Vanessa aliyecheka baada ya kuulizwa swali hilo.

“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile nyimbo ya Monefere.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX