Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » JOHARI ATESWA NA PENZI LA RAY, AFUNGUKA NA KUSEMA IPO SIKU PENZI LAO LITARUDI TU..

JOHARI ATESWA NA PENZI LA RAY, AFUNGUKA NA KUSEMA IPO SIKU PENZI LAO LITARUDI TU..

MKONGWE katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuendelea kuteseka na penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kunaswa akimzungumzia.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Viwanja vya Leaders Club kwenye uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo Johari alikuwa amekaa na kruu yake (huku wakigonga ulabu) ndipo mmoja kati wenzake hao, akagusia stori za Ray kisha Johari alicheka na kusema ipo siku Ray atarejea katika mikono yake.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’. “Ipo siku ambayo haijulikani tarehe wala mwaka Ray lazima atarudi katika mikono yangu kwani namfahamu sana Ray kuwa ni mtu wa kuruka lakini kwangu amefika,” alisikika Johari.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX