Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » KAMA UWAJUI BASI HAWA NDIYO WASANII MAARUFU DUNIANI WALIOZALIWA HAPA BONGO:

KAMA UWAJUI BASI HAWA NDIYO WASANII MAARUFU DUNIANI WALIOZALIWA HAPA BONGO:

Marin Hinkle
Wazazi wake walikutana katika moja ya harakati za kuleta amani Africa,akazaliwa nchini Tanzania,ila baadae, baada ya familia yao kumaliza mkataba wa kufanya kazi ,walirudi nchini Marekani mjini Boston,na ndipo alipokulia na kufanikiwa kwenda kusomea mambo ya sanaa chuoni.
Marin-Hinkle-copyright-vibe-co-tz
Huyu ni actress maaruf sana Hollywood,kwa wapenzi wengi wa filamu wanaweza kumgundua mapema,kupitia movie kadhaa alizowahi kucheza,katika filamu zilizowahi kuchukua tuzo na kufanya mauzo makubwa sana duniani.Amewahi kucheza kama starring msaidizi kwenye movie ya Once and Again,akacheza tena kwenye series maarufu ya Two and half Men na kuonesha kipaji chake kwenye series nyingine mpya ya Law & Order:Special Victims Unit.
Rachel Luttrell
Rachel Luttrell ni mcheza filamu na muimbaji maarufu duniani,alizaliwa hapa hapa Jijini Dar es salaam,Tanzania ,yeye akiwa ni mtoto wa kike wapili katika familia yao,baba yake akiwa ni professor wa Economics, katika chuo cha Dar es salaam.Baada tu ya kufikisha miaka mitano ,yeye na familia yake nzima ikahama nchi nakurudi kwao Canada katika jiji la Toronto.
Rachel-Luttrell-Copyright-Vibe-co-tz
Mbali na kipaji chake kizuri sana chauchezaji filamu na kuimba,Rachel ameweza kuandika story ya movie nyingi  sana,na kuweza kusaidia ku-direct yeye mwenyewe,baadhi ya movie alizowahi kucheza ni “ER”,”Sleepwalkers”,”Feast of All Saints”,”Imposter”,”Stargate Atlantis”,”I Wish You Love”,NCIS (America’s number one-rated television show) na nyingine nyingi.Ameweza kupata jina kubwa sana hapo Hollywood kwa kazi yake nzuri ya uigizaji.
Manish Patel
Huyu ni producer ,mwandishi na Director anayeheshimika sana huko nchini uingereza,amezaliwa hapa hapa Tanzania ,kati ya mpaka wa Tanzania na Zambia.Inasemekana kuwa Manish Patel ni moja kati ya wanaharakati walioweza kuinua sanaa ya filamu huko uingereza kwa kazi yake nzuri.Movie zake zimeweza kufika level za kimataifa na kuweza kuchaguliwa katika tuzo mbali mbali za filamu duniani, zikiwemo tuzo ya the Cannes Film Festival, Portobello Film Festival, Mumbai Film Festival, Bite The Mango Film Festival na nyingine nyingi. nakushinda ‘Best Film Award’ for ‘Cash and Curry’ kwenye Portobello Film Festival.
Manish-Patel-Copyright-vibe-co-tz
Freddie Mercury
Huyu ni mwimbaji nguli,mzaliwa wa huko Zenji ,Stone Town,Tanzania.Baada ya kuzaliwa kwake na kukaa kwa muda hapa nchini Tanzania, wazazi wake wakaamua kumpeleka masomoni nchini India,kwenye shule binafsi.
Freddie-Mercury-Copyright-vibe-co-tz
Baada ya muda,katika  kipindi cha masomo yake, alihamia nchini uingereza,huko ndipo kipaji chake cha kuimba kilipo onekana,alifanikiwa kwenda katika chuo cha sanaa,na huko ndipo alipokutana na wanafunzi waimbaji wenzake waliokuwa kwenye kikundi kilichokuwa kinajiita Smile. Kundi lilopata umaarufu mkubwa nchini marekani ,kufikia mauzo ya platinum ya album zao.Baada ya miaka kupita ikaja julikana kuwa Freddie alikuwa na ugonjwa usiojulikana,jambo lilomsababishia ashinde hospitali na wakati wowote apatapo nafuu hutoka na kuingia studio ku-record, haikupita muda sana,aliaga dunia,ikawa pigo kubwa katika ulimwengu wa muziki .
-Vibe

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX