Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » "KUJIUZULU KWA STEVE NTERERE NI PIGO KWA BONGO MOVIE , HAKIKA TUTAYUMBA"..MSANII CATHY AFUNGUKA

"KUJIUZULU KWA STEVE NTERERE NI PIGO KWA BONGO MOVIE , HAKIKA TUTAYUMBA"..MSANII CATHY AFUNGUKA

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.

“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.
GPL

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX