Makubwa! Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ ameangusha bonge la pati huku ikihudhuriwa na mashoga kibao.
Pati hiyo ya kufuru ambayo ilikuwa ni ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya
kijana wa mjini aliyetajwa kwa jina moja la Abdul iliyoandaliwa na Anti
Lulu ilifanyika katika Hoteli ya KB iliyopo Kijitonyama, Dar, wikiendi
iliyopita ambapo ilihudhuriwa na watu mbalimbali lakini asilimia kubwa
ya waalikwa walikuwa ni ‘wanaume tata’.
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzama ndani ‘kimafia’ ambapo
lilimshuhudia Anti Lulu akikata mauno ya kufa mtu baada ya kusikia kibao
kata kilichokuwepo hotelini hapo.
Katika pati hiyo wanawake wengi walionekana wakiwa nusu utupu na
wengine baada ya kuingia walivua nguo na kuvaa vichupi na braa kisha
kuzama kwenye bwawa la kuogelea wakifuatiwa na mashoga hao waliokuwa
wamevalia boksa na singlendi.
0 comments :
Post a Comment