Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » MCHUNGAJI AKIRI KUUZA MADAWA YA KULEVYA ...FUATILIA HAPA

MCHUNGAJI AKIRI KUUZA MADAWA YA KULEVYA ...FUATILIA HAPA

Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy lililopo Kiluvya mkoani Pwani, Nabii John Komanya (pichani), amefunguka kuwa amewahi kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kabla hajawekewa mikono na kusimikwa kuwa mtumishi wa Mungu.

Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy lililopo Kiluvya mkoani Pwani, Nabii John Komanya akiwa ndani ya Ofisi za Global.

Akizungumza katika mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili pamoja na Global Tv Online, mchungaji huyo ambaye pia ni mwanamuziki wa Injili, alisema kuwa alijiingiza kwenye biashara hiyo haramu mwaka 1996 kutokana na ushawishi wa marafiki zake ambapo alifikia hatua ya kumeza madawa hayo tumboni na kuyasafirisha nchi mbalimbali ikiwemo Malawi na Afrika Kusini.

Mchungaji huyu ambaye pia ni nabii aliye na kanisa Marekani, alisema kuwa katika kuuza madawa hayo siku moja aliweza kushuhudia marafiki zake wawili wakifariki kwa kupasukiwa madawa hayo tumboni, jambo lililomfanya afikirie upya maisha yake na kuachana nayo kisha kuamua kumtumikia Mungu.

Katika ushuhuda wake, Nabii Komanya aliongeza kuwa aliifanya kwa usiri mkubwa biashara hiyo kiasi kwamba hakuna mtu yeyote katika familia yake aliyejua kwani hakuwa akionekana kwa kuwa alikuwa mtanashati kama mtu wa kawaida.

Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy lililopo Kiluvya mkoani Pwani, Nabii John Komanya akihutubu.

“Hakuna mtu aliyekuwa akifahamu kama nilikuwa nikiuza madawa ya kulevya kwa pale nyumbani, na wala sikuwa nafanya kwa njaa kwa sababu nyumbani nilikuwa napata kila kitu kutoka kwa baba hasa kwa kuwa mimi nilikuwa mtoto pekee wa kiume katika familia.

“Hata leo hii ukiwauliza dada zangu hawatakukubalia kama niliwahi kufanya biashara hiyo ya madawa ya kulevya, kama nilivyosema nyumbani kulikuwa na kila kitu sikuwa mtu wa shida kiasi kwamba niamue kujiingiza kwenye biashara hiyo.

“ Niliamua kuachana nayo na kumtumikia Mungu na nashukuru amenijalia usikivu na nimefunguka hivi ili kuwaomba wengine kuachana na biashara hii kwa sababu wakati naifanya sikunufaika chochote kwa sababu ilikuwa ni kazi ya shetani,” alisema Mchungaji Komanya.

Nabii John Komanya akiwa na mkewe.
Mchungaji huyo ambaye anaaminika kwa kuponya watu mbalimbali kupitia muziki wake, anamiliki bendi yake inayofahamika kwa jina la Joy Band ambapo anatarajia kuzindua albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Shilo, Oktoba 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Milado uliopo Sinza jijini Dar

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX