Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » MREMBO HUYU ANAOMBA MSAADA WA MILLION TANO KWA AJILI YA MATIBABU

MREMBO HUYU ANAOMBA MSAADA WA MILLION TANO KWA AJILI YA MATIBABU

Msichana Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75.

Uvimbe huo unaomfanya alie kila mara uliifanya Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha DTV, kuwasiliana na daktari aitwaye Sabapathy wa India, aliyekubali kuifanya kazi hiyo kwa kiwango hicho cha fedha, tofauti na madai ya awali kuwa zingehitajika shilingi milioni 30.
Daktari huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo kama hayo ambaye hali yake inaendelea vyema, alisema msichana huyo atarejea katika hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini kwake na kumpangia kwa ajili ya upasuaji hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Zuhura amewaomba Watanzania kumsaidie ili kuweza kupata matatibu hayo aweze kupona na kuendelea kuwalea watoto wake ambao ni wadogo wanaohitaji msaada wake kama mama na kwamba aliyeguswa na tatizo linalomkabili anaweza kumsaidia kupitia simu yake ya mkononi namba 0717319555.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX