Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » "NIMEKOMA KUTUMIA MKOROGO"..SHILOLE AFUNGUKA

"NIMEKOMA KUTUMIA MKOROGO"..SHILOLE AFUNGUKA

MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.
Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.

“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:
“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX