Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » PICHA ZA SERENGETI FIESTA SHINYANGA NI SHEEDAAAAHHHH

PICHA ZA SERENGETI FIESTA SHINYANGA NI SHEEDAAAAHHHH




Pichani kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.


Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wakazi wa mji huo usiku katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage

Mmoja wa wasanii wa Bongofleva anaefanya vyema katika muziki huo atambulikae kwa jina la Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.


Pichani juu na chini ni umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.

Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia) na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga .

Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mwanadada Linah akionesha umahiri wake wa kucheza wimbo wake wa Ole Temba juu ya jukwaa la Fiesta 2014 kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.

Ukipenda muite Mr Blue,msanii wa muziki wa kizazi kipya juu ya jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.





Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.





Mmoja wa wakali wa kukamua mangona kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua ngoma jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Shinyanga kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage

Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika .
-freebongo

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX