Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » UKATILI: BABA AMUUA MPENZI WAKE KIUKATILI NA KUMTUPA KWENYE KORONGO

UKATILI: BABA AMUUA MPENZI WAKE KIUKATILI NA KUMTUPA KWENYE KORONGO



Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.


Taarifa za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume mahakamani na kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jela. Siku kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi wake huyo aliyesababisha kuwekwa ndani anatembea na mwanaume mwingine ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.


Taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20:13 alimwambia mpenzi wake kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari" Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha.


Mara baada ya mwaume kufanya unyama huo inasemekana zilipita siku kadhaa ndipo mwanaume alipowapiga simu kwa ndugu wa mwanamke huyo; "Njooni mchukue mzoga wenu!" Aliongea mwanaume huyo.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX