Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » , » Wema Sepetu 'Watu Wenye Majungu Hawanisumbui Kichwa Kabisa Nabaki Nawatazama Tu'

Wema Sepetu 'Watu Wenye Majungu Hawanisumbui Kichwa Kabisa Nabaki Nawatazama Tu'


Stori: Mayasa Mariwata
MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi.

Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.

“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX