Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » , » BIRTHDAY YA DIAMOND, BEATIFUL ONYINYE WEMA SEPETU AZUA GUMZO!..TAZAMA PICHA NA VIDEO YA KILICHOTOKEA

BIRTHDAY YA DIAMOND, BEATIFUL ONYINYE WEMA SEPETU AZUA GUMZO!..TAZAMA PICHA NA VIDEO YA KILICHOTOKEA

Stori: Waandishi Wetu
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’.
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Diamond Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya pamoja.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake.
Saa 3:30 USIKU
BUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei.
SAA 4:00 USIKU
BIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh! Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani.
SAA 5:00 USIKU
SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
Nuh Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo.
Risasi Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKU
NGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Wageni waalikwa wakizidi kuingia ukumbini.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki ya Bethidei ya Diamond.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX