MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha Bongo, Baby
Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila
kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’
kama angekuwa yeye.
Mwanamuziki mwenye vituko kila kukicha Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond
anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na
kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua
ya kuwaonea wivu.
“Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati
natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa
Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.
0 comments :
Post a Comment