MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata baada ya kupiga picha akiwa ametinga suruali iliyochanika.
Akizungumzia picha hiyo ambayo imevuja
katika baadhi ya mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi
karibuni Afrika Kusini alipokuwa amekwenda kurekodi wimbo wake mpya
(hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili kuonesha utofauti.
“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata watu wengi walikuwa wakijiuliza
kulikoni mimi kuvaa hivyo lakini mimi nafikiri lazima kuna wakati
tunatakiwa kuonekana tofauti na siyo mapambo muda wote ukibadilika hata
unachofanya unakuwa tofauti,” alisema Jokate
0 comments :
Post a Comment