Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » , » Meninah Aongelea Issue ya Yeye Kufunga Ndoa na Mwanamuziki Diamond Platnumz

Meninah Aongelea Issue ya Yeye Kufunga Ndoa na Mwanamuziki Diamond Platnumz


"Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.

“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo ambalo si la kweli.”

“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.” Meninah

Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.


0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX