Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Simu za iphone 6 Kimenuka, Watumiaji wa Simu Hizo Walalamika Zinapinda

Simu za iphone 6 Kimenuka, Watumiaji wa Simu Hizo Walalamika Zinapinda


Watafiti wamechanganyikiwa kuhusu ikiwa kampuni ya Apple inapaswa kutoa kauli yake kuhusu ripoti kuwa simu yake mpya ya iPhone 6 inajipinda mtumiaji anapoishi kuiweka ndani ya mfuko wa suruale yake.
Watu kadhaa ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao kwenye mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa na tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa 'Geek.com' pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX