Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Afande Sele Anaswa na Demu Mpya..Mwenyewe Adai ni Maswala Yake Binafsi Asiulizwe

Afande Sele Anaswa na Demu Mpya..Mwenyewe Adai ni Maswala Yake Binafsi Asiulizwe


MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, juzikati alinaswa akiwa na demu mpya akiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika kwa 40 ya aliyekuwa mzazi mwenzake, marehemu mama Tunda.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Septemba 21 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati staa huyo aliyekuwa mmoja wa watoa burudani katika tamasha la Fiesta, alipoonekana akiingia akiwa ameambatana na mrembo mmoja akiwa ameshikana naye kimahaba.

Akiwa ndani ya uwanja huo, mkali huyo wa mashairi yenye vina kwa muda mwingi alikuwa pamoja na msichana huyo ambaye hakufahamika jina, wakiwa na dalili zote za wapendanao.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, Afande Sele alicheka na kumtaka paparazzi wetu kuachana na masuala hayo aliyoyaita binafsi, badala yake asubiri apande jukwaani apate picha za kazi atakayofanya.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. BONGO STARS LINK - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX