Msanii wa Muziki wa Bongo
Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala
katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar akihusishwa na utekaji wa
dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa kipigo ambapo
inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi.
Baada ya
tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa
picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja
wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa
wake Madee alikiona cha mtemakuni.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni,
nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja
akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka
mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila
inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru
baada ya kulala selo,” kilidai chanzo hicho.
Kufuatia msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake
Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua
simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe ndipo Madee alipomtaiti Suedi
na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa polisi kwa kufunguliwa kesi
iliyosomeka: VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA BINADAMU
0 comments :
Post a Comment