Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake aliyefariki dunia juzikati.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za mdogo
wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki
dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye mazishi.
Ijumaa lilipata bahati ya
kuwasiliana na Aunt ambaye alisema ameshitushwa na taarifa hizo na
alikuwa njiani kurejea Dar.“Nimeumia sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu
tuliyependana sana lakini Mungu kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa
masikitiko.
0 comments :
Post a Comment