BAADA
ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa
na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na
kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos
‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu
msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya
Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati
alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane
milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu
waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla
hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane
milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu
hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa
sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko
japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama
Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na
kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla
ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa
imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua
Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.

Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:
“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.”

0 comments :
Post a Comment